Siku ya Ijumaa, Mbunge wa chama cha Democrat Betty McCollum aliwasilisha tena muswada ambao utakataza msaada wa Marekani hautumiki kuwaweka kizuizini watoto wa Kipalestina na hautumiki katika shughuli za kijeshi ambazo zingewezesha "kutekwa zaidi "Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.
"Si dola moja ya msaada wa Marekani inapaswa kutumika kufanya ukiukaji wa haki za binadamu, kubomoa nyumba za familia, au kunyakua kabisa ardhi ya Wapalestina," McCollum alisema katika taarifa yake.
"Marekani hutoa msaada wa mabilioni kwa serikali ya Israeli kila mwaka - na dola hizo zinapaswa kuelekea 'usalama' wa Israel, sio kwa vitendo vinavyokiuka sheria za kimataifa na kusababisha madhara."
Utawala haramu wa Israel unayoshutumiwa kwa ubaguzi wa rangi na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na Amnesty International, inapokea angalau dola bilioni 3.8 kama msaada kutoka serikali ya Marekani kila mwaka.
Mswada huo uliopewa jina la Kutetea Haki za Kibinadamu za Watoto wa Kipalestina na Familia Zinazoishi Chini ya Sheria ya Ukaliaji Kijeshi wa Israel, una nafasi ndogo ya kupitishwa katika Bunge la Congress, ambako utawala wa Kizayuni wa Israel unaungwa mkono mkubwa na pande mbili za Democrat na Republican.
Kulingana na ripoti kati ya watoto 500 na 700 wa Kipalestina, wenye umri wa miaka 12 hadi 17, wanazuiliwa na Israel kila mwaka na kufunguliwa mashtaka mbele ya mahakama za kijeshi za utawala huo ambao ni maarufu kwa kuwaua watoto kiholela.