IQNA

Qiraa

Qari wa Iraq akisoma aya za Surah Al Imran wakati wa Krismasi (+Video)

12:40 - May 14, 2023
Habari ID: 3476996
TEHRAN (IQNA) – Katika mnasaba wa Krismasi, ambayo ni siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Nabii Issa Masih au Yesu (AS), qari wa Iraq alisoma aya kutoka katika Surah Al Imran ya Qur’ani Tukufu.

Hadhrat Maryam, mama yake Isa (AS), ametajwa katika Qur'ani Tukufu kuwa ni mwanamke mwema, ambaye hakuwa mtume bali alilelewa kama mtume na ambaye mwenendo wake ulikuwa kama ule wa mitume wa Mwenyezi Mungu.

Qari wa Iraq, Hassan al-Zabhawi, alisoma aya ya 37 ya Surah Al Imran, ambayo inazungumza juu ya riziki ya Mwenyezi Mungu iliyotumwa kwa Hazrat Maryam (SA):

“Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.”

captcha