IQNA

Qur'ani Tukufu

Usajili wa Mpango wa Kitaifa wa Qur'ani Tukufu wa Amir Al-Qurra nchini Iraq

21:20 - May 14, 2023
Habari ID: 3477001
TEHRAN (IQNA) – Usajili wa toleo la 7 la mpango wa kitaifa wa Qur'ani Tukufu kwa vijana nchini Iraq ulianza Alhamisi na utahitimishwa leo.

Mpango huo unaojulikana kama  Amir al-Qurra (mfalme wa wasomaji wa Qur'ani), imeandaliwa na Majlisi ya Kisayansi ya Qur'ani Tukufu yenye uhusiano na Mfawidhi wa Kaburi Takatifu la Hadhrat Abbas (AS).

Wale kutoka kote Iraq walio tayari kushiriki katika tukio la Qur'ani wanatakiwa kuwasilisha faili ya video ya usomaji wao wa Qur'an kwa mtindo wa Iraqi au Misri.

Waombaji hawapaswi kuwa zaidi ya miaka 17, kulingana na kanuni, tovuti ya Al-Kafeel iliripoti. Mpango huo hutekelezwa kila mwaka wakati wa kiangazi wakati shule zimefungwa.

Vijana wanaohitimu kushiriki katika mpango huo hukusanyika katika mji mtakatifu wa Karbala ili kujifunza na kuimarisha ujuzi wao katika usomaji wa Qur'ani Tukufu.

Wanachukua kozi zilizoandaliwa na Majlisi ya Kisayansi ya Qur'ani Tukufu chini ya usimamizi wa mabwana na wataalamu wa Qur'ani.

Kubainisha vipaji vya Qur'ani vya Iraq na kuwafunza katika nyanja ya usomaji wa Qur'ani ni miongoni mwa malengo ya mpango huo.

 4140622

 

captcha