IQNA

Haram Takatifu ya Bibi Maasuma (SA) yapambwa kwa Maelfu ya Maua

QOM (IQNA) - Haram Takatifu (kaburi) ya Bibi Maasuma (SA) huko Qom, Iran imepambwa kwa maelfu ya maua siku ya Ijumaa kuadhimisha sherehe za Karamat.

Sherehe za Karamat zinaadhimisha siku kumi kati ya kumbukumbu za kuzaliwa Bibi Maasuma (SA) na Imam Ridha (AS), binti na mtoto wa Imam Mussa bin Jaafar al-Kadhim AS Imam wa saba wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia.