IQNA

Harakati za Qur'ani

Vituo vya Qur'ani vya kuhudumia wanaozuru Haram ya Imam Kadhim (AS) nchini Iraq

19:49 - February 02, 2024
Habari ID: 3478290
IQNA - Vituo kadhaa vya Qur'ani vimejengwa kwenye njia ya mamilioni ya wafanyaziara wanaotaka kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Musa Kadhim (AS) nchini Iraq.

Mamilioni ya wafanyaziara wanamiminika katika eneo la Kadhimiya nchini Iraq kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Musa Kadhim (AS), Imam wa saba wa Madhehebu ya Shia, katika siku ya 25 ya mwezi wa Hijri wa Rajab (Jumanne, Februari 5, 2024).

Idara ya Mfawidhi wa Harama ya Hadhrat Abbas (AS) imeandaa vituo kadhaa vya Qur'ani njiani ili kutoa programu mbalimbali ambazo zinasimamiwa na wataalamu 15 wa Qur'ani.

Programu hizo ni pamoja na kufundisha usomaji sahihi wa Qur'ani Tukufu, kufundisha kuhifadhi sura fupi za Qur'ani Tukufu, dua, na kujibu maswali kuhusu Qur'ani.

Imam Kadhim (AS) alilishwa sumu na kuuawa kishahidi mnamo tarehe 25 Rajab, 183 Hijria (Septemba 5, 799 CE) katika jela huko Baghdad. Haram  yake takatifu iko Kadhimiya, kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq.

Maafisa wa serikali  wanatarajia wafanyaziara milioni kumi kutoka Iraq, Iran, India, Pakistan, Lebanon na nchi zingine kuutembelea mji huo mtakatifu katika siku chache zijazo.

Waziri mkuu wa Iraq aimeamuru kuundwa kwa kamati ya kuhakikisha usalama na kutoa huduma muhimu kwa wafanyaziara

Wizara ya afya ya Iraq pia imetuma magari ya kubebea wagonjwa kwenye barabara zinazoelekea katika eneo hilo takatifu ili kutoa dawa na vifaa vya matibabu.

Zaidi ya hayo, wizara ya afya itasimamia usambazaji wa vyakula na vinywaji ili kuhakikisha kuwa viwango vya afya vinazingatiwa.

3487052

captcha