IQNA

Maadili katika Qur'ani / 6

Chimbuko na Aina za Usaliti

17:42 - June 19, 2023
Habari ID: 3477161
Uhaini ni miongoni mwa sifa zisizofaa ambazo Qur’ani Tukufu inazizungumzia, Kitabu kitukufu pia kinazungumzia aina mbalimbali za khiana.

Usaliti ni miongoni mwa tabia zinazodhoofisha msingi wa jamii na katika vyanzo vya kidini, watu wameonywa dhidi yake. Uhaini ni kudhoofisha na kuharibu uaminifu wa mtu. Moja ya sababu za msingi za khiana ni Nafisi Ammarah (mtu anayechochea). Nafisi Ammarah humfanya mtu kutotumia akili yake na hivyo anafanya makosa na kufanya madhambi. Nabii Joseph (AS) aliitaja Nafisi Ammarah kama sababu ya kile Zuleikha alichofanya. Lakini mimi sioni nafsi yangu kuwa haina hatia, hakika nafsi inachochea maovu isipokuwa ambaye Mola wangu Mlezi amemrehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu, Mwenye kurehemu, Tafsiri ya  Aya ya 53 ya Surati Yusuf.

Sababu nyingine ya msingi ya khiana ni Shirki (ushirikina) na ukosefu wa imani katika uwezo wa M wenyezi  Mungu, Wale walio dhaifu katika imani nyakati fulani hufanya hiana kwa sababu wanafikiri kwamba vinginevyo wataanguka nyuma ya wengine na maslahi yao hayatatumikiwa. Kwa mujibu wa Quran Tukufu  khiana inaweza kuwa ya aina tofauti; 1- Kumsaliti Mwenyezi Mungu na Mtume (S.aw.w.);  Tafsiri ya Aya katika Qurani Tukufu  imeharamisha kumsaliti Mwenyezi Mungu na Mtume Mtukufu (S.aw.w.);  Enyi mlioamini, msimfanyie khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini mliyokabidhiwa hali mnajua Tafsiri ya  Aya ya 27 ya Surati Anfal.

2- Usaliti wa watu, Katika Aya hii hii, Mwenyezi  Mungu pia ametuamrisha tuwe waangalifu sana juu ya mambo uliyokabidhiwa, Kwa mujibu wa Hadiyth kutoka kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), kuna mambo manne ambayo ikiwa moja kati yao litaingia kwenye nyumba au jamii, nyumba hiyo au jamii hiyo haitapata baraka za Mwenyezi Mungu, Na mambo hayo manne ni khiana, wizi, unywaji wa mvinyo na uzinzi. Dawa mojawapo ya ugonjwa huu wa kimaadili (usaliti) ni kuimarisha imani ya mtu.  Mtu lazima pia atafakari juu ya matokeo ya usaliti, ambayo ingemfanya atambue kwamba lazima aepuke.

 

 

3483988

Kishikizo: usaliti
captcha