IQNA

Tani 400 za Maji ya Zamzam Husafirishwa kutoka Makka hadi Madina Kila Siku wakati wa Hija

9:48 - June 27, 2023
Habari ID: 3477201
Tani 400 za maji ya Zamzam hutolewa kwa Msikiti wa Mtume huko Mjini Madina kila siku wakati wa msimu wa Hija.

Maji hayo husafirishwa kutoka Makka  kila siku, Shirika la Habari la Saudi (SPA) lilitoa ripoti.

Maji matukufu  hutiwa ndani ya vyombo 10,000 ambavyo vinapatikana karibu na msikiti, na kontena 5,000 za ziada hutumika ikiwa inahitajika.

Wafanyikazi na wasimamizi wapatao 530 wanahusika katika kujaza makontena hayo na kuyahamishia katika maeneo waliyopangiwa  ya kwenda  misikitini   juu ya paa lake na katika ua wake.

Maeneo saba katika msikiti huo yalitengwa kwa ajili ya kujaza vyombo na maeneo matatu yalitumika kupoza chupa za maji za Zamzam zinazotumika mara moja, 80,000 kati yake zikisambazwa kila siku, iliongeza ripoti hiyo.

Saudi Arabia inatarajia zaidi ya mahujaji milioni mbili kutoka zaidi ya nchi 160 wakati wa msimu huu wa Hija baada ya kuondolewa kwa vikwazo vinavyohusiana na janga la Corona Yani COVID-19.

Hija ya kwenda Makka ni wajibu wa lazima wa kidini ambao lazima utekelezwe na wale Waislamu ambao wana uwezo wa kimwili na wa kifedha kuitekeleza, angalau mara moja katika maisha.

 

3484072

 

Kishikizo: maji ya zam zam
captcha