IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Rais wa Iran katika UN: Maadui hawatafanikiwa kamwe kupotosha ukweli wa Qur'ani Tukufu

20:30 - September 20, 2023
Habari ID: 3477623
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa Iran amelihutubia Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kueleza kwamba, maadui hawatafanikiwa kupotosha uhakika wa Qur'ani Tukufu.

Rais wa Iran ameyanyua juu kitabu cha Qur'an na kuwapa ujumbe walimwengu kwa kusema: "Qur'an hii ni yenye mafunzo adhimu sana, ni Kitabu kinachotengeneza utamaduni mzuri wa Mwanadamu, ni Kitabu Kitukufu kinachomtengeneza vyema Mwanadamu, ni kitabu chenye kutengeneza jamii ya mwanadamu, ni kitabu cha milele, na kuupotosha ukweli wa Qur'an ni kitu ambacho hakiwezekani, hii Qur'an huwezi kuichoma moto na kuipoteza abadan"...

Akilaani vitendo vya karibuni vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Uswidi na Denmark Rais wa Iran amesisitiza kuwa, "Tunaamini kuwa, kuheshimiwa matukufu ya kidini kunapasa kuwa moja ya ajenda kuu za Umoja wa Mataifa."

Kwingineko katika hotuba yake, Rais Ebrahim Raisi  amesema mpango wa Marekani wa kuitwisha dunia sera na misimamo yake umefeli na kugonga mwamba.

Ameengeza kuwa, "Dunia inaelekea katika nidhamu mpya ya kimataifa, na mradi wa kuufanya ulimwengu uwe wa Kimarekani umefeli."

Amesema taifa la Iran kwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu linajifakharisha kwa kuwa na nafasi kubwa katika kuwaanika mabeberu Mashariki na Magharibi.

Rais wa Iran amebainisha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inathamini mno usalama wa nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi na kusisitiza kuwa, uwepo wa maajinabi katika eneo si sehemu ya suluhu, bali ni tatizo na uwepo huo unayazidisha mashaka mataifa ya Asia Magharibi.

"Jamhuri ya Kiislamu inakaribisha na kuupokea kwa moyo mkunjufu mkono wa urafiki ikiamini kwa dhati kwamba, uhuru na ujirani mwema unatoa fursa zenye maslahi kwa eneo zima, " ameongeza Sayyid Raisi. 

Ameashiria vita vya Ukraine na umuhimu wa kutumia diplomasia kutatua mgogoro huo na kusema: Msimamo wetu ulio wazi kama Jamhuri ya Kiislamu ni kwamba, hatuungi mkono vita vyovyote popote pale duniani ikiwemo Ulaya.

Aidha amelipongeza taifa la Iran kwa kusimama kidete mkabala wa njama za maadui walioibua na kuchochea ghasia mwaka jana hapa nchini, kwa kisingizio cha kifo cha mwanamke wa Kiirani, Mahsa Amini.

Rais wa Iran amesema bayana kuwa: Taifa la Iran liliweza kuzima hujuma kubwa zaidi ya vyombo vya habari na vita vikubwa zaidi vya kisaikolojia katika historia.

4169955

Habari zinazohusiana
captcha