IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Mataifa ya Kiislamu yanapaswa kudiriki uwezo wao wa kiuchumi na kuimarisha umoja

16:49 - August 03, 2023
Habari ID: 3477373
TEHRAN (IQNA) - Msomi wa Malaysia anasema ili kujibu kiuchumi mashambulizi ya Wamagharibi dhidi ya Uislamu na Qur'ani Tukufu, mataifa ya Kiislamu yanahitaji kuelewa uwezo wao na kujenga umoja.

Muhammad Azmi Abdulhamid, rais wa Baraza la Ushauri la Mashirika ya Kiislamu ya Malaysia (MAPIM) aliyasema hayo alipokuwa akihutubia katika semina ya mtandaoni iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani (IQNA) ambayo imefanyika kwa njia ya intaneti chini ya anuani ya "Qur'ani, Kitabu chenye nguvu na utukufu" kwa kushirikisha wanachuo kutoka nchi mbalimbali siku ya Jumanne. Kikao hicho kilisimamiwa na Sayyid Abbas Anjam, msomi maarufu wa Qur'ani Tukufu nchini Iran.
Baadhi ya watu wa nchi za Magharibi "wameuelewa vibaya" Uislamu kutokana na jinsi dini hiyo inavyosawiriwa na vyombo vya habari vya Magharibi, alisema, akiongeza kuwa vyombo vya habari vinajaribu kuashiria kwamba Qur'ani Tukufu "ni kinyume na kile wanachokiita haki za binadamu".
Ulimwengu wa Kiislamu bado "haujawa na nguvu za kutosha" kujibu kiuchumi vitendo vya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu. Nchi za Kiislamu zimeshindwa kuungana katika masuala ya uchumi, alisikitika na kuongeza kuwa nchi za Kiislamu zinategemea uchumi, teknolojia na biashara ya Magharibi. ..
Ametaja njia tatu zinazoweza kutumika kuufanya Umma wa Kiislamu kuwa na nguvu zaidi kiuchumi amesema
Kwanza kabisa, aliendelea, "Tunahitaji kusoma uwezo wa uchumi wa mataifa ya Kiislamu ... tuna rasilimali nyingi, tuna rasilimali watu bilioni mbili/ Pia tuna rasilimali nyingi ndani ya nchi. Tuna madini, tuna mafuta. Tunaweza kutumia utajiri huu kujibu mashambulizi yoyote dhidi ya Uislamu."
Akiashiria matumizi ya bidhaa za nchi za Magharibi katika mataifa ya Kiislamu, mwanazuoni huyo alisema "Tunaweza kuanzisha mgomo wa kiuchumi" ili kutuma "ujumbe mkali kwa madola ya Magharibi."
Na hatimaye, aliashiria haja ya "kuelewa zana kuu za kiuchumi tulizo nazo miongoni mwa Waislamu... Hatutumii mtaji kwenye mfumo wetu ambao una nguvu za kutosha kuwa na aina ya njia mbadala."
"Tunasimamia vibaya mali zetu," alisema na kuongeza kuwa utajiri mkubwa wa mataifa ya Kiislamu hausaidii masuala kama vile Palestina na badala yake "unawanufaisha maadui wa Uislamu na wana uwezo wa kutukandamiza kwa kutumia uchumi."

3484611

 

Habari zinazohusiana
captcha