
Miongoni mwa maduka ya Sheikh Rizwan Bazaar, alama kubwa iliwekwa miongoni mwa alama za maduka madogo ya karibu, ambayo huvutia hisia zaidi na iliandikwa, Kituo cha Hifadhi ya Qur'ani Tukufu Mkabidhi Qur’ani Tukufu yako ya zamani na Upokee na Qur’ani mpya bila malipo.
Jabr alichagua duka hili, ambalo alipewa na Manispaa ya Gaza, katikati ya bazaar, ambapo watu wanaweza kuipata kwa urahisi.
Jabr, pamoja na rafiki yake na msaidizi wake, Rajab Salman mwenye umri wa miaka 65, huja asubuhi na mapema na kuanza kufanya kazi ndani ya duka na vitu rahisi vilivyotengenezwa kwa mikono ilivyotolewa na watu wema.
Alisema kwamba wazo la kukarabati na kurejesha Qur’ani Tukufu za zamani lilimjia akilini takriban miaka 10 iliyopita, baada ya kuona karatasi nyingi za Qur'ani zilizopatikana katika sehemu ambayo ilikuwa imeharibiwa kwa njia isiyo sahihi, pamoja na Qur'ani kuachwa majumbani bila kurejeshwa Misikiti na sehemu nyengine zimechakaa.
Aliongeza kwa kusema; Hapo awali tulikuwa tunaweka masanduku misikitini kwa ajili ya kukusanya Qur’ani zinazohitaji kutengenezwa, kisha tukayaweka kwenye ghala hadi tulipopewa nafasi na manispaa, tukaanza kufanya kazi bure kupeleka hizi Qu’rani ili zirudishe wamiliki wao au kuwapa wengine kwa idhini ya wamiliki wao.
Jaber aliendelea kwa kusema; Kuna mahitaji mengi kutoka kwa watu kurejesha Qur’ani zao, tulipokea na kutoa baadhi ya nakala za Qur'ani karibu kila siku, na nakala nyingi zilizoletwa kwetu zilikuwa na vifuniko vilivyochanika au karatasi au watoto waliandika na kalamu.
Alieleza kuwa kazi ya kurejesha Qur’ani ilihitaji umakini mkubwa ili kuhakikisha kwamba hakuna ukurasa unaoachwa hasa kwa vile kazi hii inafanywa kwa zana rahisi na za msingi kama vile gundi, kadibodi, nguo, penseli ya mkono na mkasi.
Mfadhili huyo wa Kipalestina alisisitiza; Wanavyuoni walijitahidi sana kuihifadhi Qur'ani Tukufu hii kwa namna hiyo nzuri na sahihi kwa ajili yetu, na hata leo sisi hatufanyi ubakhili katika kuitunza bila malipo na kwa ikhlasi, na malipo yetu yanatoka kwa Mwenyezi Mungu.