IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya Kwanza ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Kazakhstan yamalizika

18:50 - November 03, 2023
Habari ID: 3477834
ASTANA (IQNA) - Mwakilishi kutoka Morocco alishinda tuzo ya juu ya Mashindano ya Kwanza ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Kazakhstan.

Sherehe ya kufunga, ambayo ilifanyika Alhamisi katika Msikiti Mkuu wa Astana katika mji mkuu wa Astana, iliashiria mwisho wa hafla hiyo ya siku mbili.

Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani yameshuhudia ushiriki wa wahifadhi 30 kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Indonesia, Malaysia, Iran, UAE, Saudi Arabia, Marekani, Misri, Uturuki, Russia, Kuwait na Guinea kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya Kazakhstan.

Washindi sita bora wa shindano hilo walitangazwa kama ifuatavyo:

- Ilyas Hajri kutoka Morocco alipata nafasi ya kwanza na kutunukiwa US$ 20,000.

- Turpal-Ali Sadykov kutoka Chechnya alishika nafasi ya pili na kupokea zawadi ya pesa taslimu US$ 15,000.

- Malek Abdullah Albadin kutoka Libya na Saad Salim kutoka Algeria wote walipata nafasi ya tatu, kila mmoja akipokea dola US$ 7,000.

- Abdurahman Faraj Hafiz Baragi kutoka Misri alipata nafasi ya nne na kutunukiwa zawadi ya pesa taslimu $5,000.

- Muhammad Adib bin Ahmed Razani kutoka Malaysia alipata nafasi ya tano, akipokea zawadi ya pesa taslimu $3,000.

Hafla hiyo iliandaliwa na Utawala wa Kidini wa Waislamu wa Kazakhstan kuadhimisha Siku ya Jamhuri, sikukuu muhimu ya kitaifa.

Jopo la majaji lilijumuisha wataalamu mashuhuri wa Qur'ani, akiwemo Hafiz Othman Shahin kutoka Uturuki, Mahir Farmawi kutoka Misri, Jahangir Nematov kutoka Uzbekistan, Abdullah al-Hashimi kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, na Yarsin Amir kutoka Kazakhstan.

4179503

captcha