IQNA

Kazakhstan yakosolewa kwa kumtoza faini muigizaji aliyenukuu Qur’ani

18:04 - September 27, 2024
Habari ID: 3479496
IQNA- Serikali ya Kazakhstan imekosolewa kwa kumtoza faini mwigizaji kwa kunukuu kutoka kwa Qur'ani Tukufu katika chapisho la Instagram.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR), shirika kubwa zaidi la kutetea haki za Waislamu nchini  Marekani limelaani hatua hiyo katika taarifa iliyotolewa Alhamisi.

Mwigizaji na mtayarishaji Nurtas Adambay anadaiwa eti alikiuka sheria za Kazakhstan kuhusu shughuli za kidini na vyama kwa kusambaza maudhui ya kidini bila kibali kinachofaa. Imedaiwa kuwa aya za Qur’ani nchini humo zinatumika tu katika maeneo fulani kama vile misikiti na shule za kidini.

"Uhuru wa kidini ni haki ya msingi ya watu wote duniani kote," alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kitaifa wa CAIR Ibrahim Hooper.

"Tunalaani kitendo hiki cha kimabavu cha serikali ya Kazakhstan na tunaomba faini iondolewe na sheria isiyo ya haki ibadilishwe ili kuruhusu uhuru wa kweli wa kujieleza."

Aliongeza kwamba “ijapokuwa washiriki wa mashirika mengi ya kidini yaliyosajiliwa waliweza kufuata dini bila bughudha au vizuizi vya kisheria ndani ya majengo ya ibada yaliyosajiliwa na nyumba za kibinafsi, wenye mamlaka waliendelea kuwatoza faini, kuwakamata, kuwaweka kizuizini, au kuwafunga wananchi kwa sababu ya imani yao ya kidini au ushirika wao nchini Kazakhstan.”

3490051

captcha