
Fatima Amarneh, ambaye alikamatwa na kupigwa vibaya na askari vamizi wa Israel takriban miezi miwili iliyopita kwa madai ya "kujaribu kumchoma kisu" karibu na Msikiti wa Al-Aqsa, alizungumza na vyombo vya habari siku ya Ijumaa baada ya kuwasili katika nyumba ya familia yake katika mji wa Ya'bad karibu na Jenin kaskazini mwa eneo linalokaliwa kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi
"Israel iliweka vikwazo vya ziada kwa wafungwa wa kike baada ya Oktoba 7," Amarneh alisema. "Israel ilichukua kila kitu kutoka kwa wafungwa wanawake licha ya kuwa tayari walikuwa wanakosa chakula, blanketi, nguo, na zaidi ya uhuru wote."
"Pamoja na kukamatwa kwangu, kuuhifadhi na kuutetea Msikiti wa Al-Aqsa ni heshima, kwani ndio msingi wa maisha ya Muislamu," aliongeza.
Amarneh alikuwa mmoja wa Wapalestina 39 walioachiliwa kutoka jela za kuogofya za Israel siku ya Ijumaa, siku ya kwanza ya kusitishwa kwa vita baada ya ya Waisraeli 24 na wageni waliokuwa wakishikiliwa na Hamas kuachiliwa huru.Mkataba wa kubadilishana wafungwa, uliopatanishwa na Qatar na Misri, unatarajiwa kuendelea kwa siku nne zaidi.
Makubaliano hayo yanakuja baada ya takriban siku 50 za mashambulizi ya kikatili ya utawala dhalimu wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza uliozingirwa ambayo yalisababisha vifo vya Wapalestina 14,854 wakiwemo watoto 6,150 na zaidi ya wanawake 4,000.
Hujuma hiyo ya Israeli ilianza baada ya makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina yakiongozwa na Hamas kuanzisha operesheni kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu Oktoba 7 ili kukabiliana na miongo kadhaa jinai za Israel. Mashambulizi hayo yaliuawa takriban wanajeshi 1,200 wa Israel na walowezi wa Kizayuni. Taarifa zinasema wanajeshi wa Israel waliouawa lakini utawala wa Tel Aviv unaficha ukweli.
3486155