Musharraf Hussain, ambaye kazi yake "Qur’ani Tukufu: Tafsiri ya Kiingereza Sahali" ilichapishwa mnamo 2018, aliiambia Al Jazeera kwamba Waislamu wapya au waliosilimu katika nchi za Magharibi wameonyesha nia hasa ya kusoma tafsiri za Kiingereza za Qur’ani Tukufu ili kuelewa vyema mafundisho ya Uislamu.
Amesema tangu vita vya mauaji ya halaiki ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza vilipoanza mwezi Oktoba 2023, mauzo ya tafsiri yake yameongezeka maradufu katika muundo wa maandishi na wa kidijitali.
Hussain alisema ametumia lugha iliyo rahisi kueleweka katika tafsiri yake ili kuwasaidia Waislamu waliosilimu na wale wanaofikiria kuukubali Uislamu kuelewa vyema dhana za Qur'ani.
Alibainisha kwamba ameepuka mbinu ya wafasiri waliotangulia ambao waliegemea tafsiri ya neno kwa neno ya aya.
Alisema amepokea mamia ya maoni chanya kutoka kwa wale wanaosoma tafsiri yake.
Kulingana na Hussain idadi ya taasisi za kidini, ikiwa ni pamoja na Dar al-Ifta ya Misri, pamoja na wanazuoni wengi na watafiti, wameidhinisha tafsiri yake.
Kwingineko katika matamshi yake, alisisitiza umuhimu wa kuwaunga mkono watu wa Gaza na kuwawekea mashinikizo wanasiasa ili wasitishe vita vya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya kambi ya Palestina.