IQNA

Nidhamu Katika Qur’an/13

Nidhamu ya kijamii katika Uislamu

23:23 - May 13, 2024
Habari ID: 3478817
IQNA – Kile Uislamu unasema kuhusu nidamu ya kijamii ni mbali zaidi ya kile ambacho wengine wanasema. Kwa mujibu wa Uislamu, nidhamu ya kijamii uinapaswa kuwa kiasi kwamba haina madhara kwa uhuru wa mtu binafsi na uadilifu wa kijamii.

Jamii inapaswa kuweka misingi ya watu binafsi kufikia furaha duniani na akhera. Jamii kama hiyo inahitaji sheria sahihi na zilizobainishwa. Kwa hakika, kutokana na mapungufu , ubinadamu hauwezi kufikia sheria zinazoweza kutumika wakati wote na mahali popote isipokuwa kuwe na uhusiano na Mwenyezi Mungu.

Kwa upande mwingine, kuanzisha utulivu katika jamii bila kuwepo kwa watu wanaotetea sheria na haki za kibinafsi na za kijamii ni jambo lisilowezekana. Mojawapo ya dhihirisho la nidhamu katika jamii ni kutimiza ahadi.

Qur’ani Tukufu inasema katika Aya ya 8 ya Surah Muminun: “(Wamefanikiwa) ambao wanahifadhi amana zao na ahadi zao.”

Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) alisema mtu ambaye si mkweli wa ahadi zake si muumini.

Pia imesisitizwa katika Hadithi kwamba mtu asiangalie ni kiasi gani watu wanaswali au kufunga ili kuhukumu kiwango cha imani yao, bali ni jinsi gani walivyo waaminifu kwa ahadi zao.

Katika dakika za mwisho za maisha yake, Mtukufu Mtume (SAW) alimwambia Imam Ali (AS) kurudisha kile alichokabidhiwa, bila kujadli iwapo mmiliki wake ni mtu mwadilifu au mtenda maovu na hata kiwe kidogo kiasi gani.

Mtukufu Mtume (SAW.) alikuwa mwangalifu hata kuhusu mambo madogo madogo kuhusu kutumiza ahadi. Siku moja mtu mmoja alimwambia Mtume (SAW) amngojee karibu na jabali. Baada ya muda, jua lilianza kumsumbua. Wenzake wakamuuliza kwanini hasogei kivulini, akasema sehemu aliyoahidiwa kusubiri ni pale alipokuwa amesimama na si kivulini.

3488224

Kishikizo: jamii qurani tukufu
captcha