Kwa mujibu wa Al-Kafeel, jukwaa hilo linaendeleza mfululizo wa shughuli za Qur’ani sambamba na huduma mbalimbali kwa wafanyaziyara wa Arbaeen katika mkoa huo.
Kituo cha Qur’ani cha jukwaa kimeweka vituo kadhaa vya Qur’ani kando ya barabara zinazoelekea Karbala.
Zaidi ya wasomaji na wahifadhi wa Qur’ani 40 wamepelekwa kwenye vituo hivyo, wakifundish wafanyaziyara usomaji sahihi wa Surah Al-Fatiha na Surah fupi, pamoja na kuwasaidia kurekebisha usomaji wa sala zao.
Hatua hii inalenga kuhakikisha usahihi wa utekelezaji wa Sala na kuongeza uelewa wa kidini miongoni mwa wafanyaziyara.
Kituo hicho pia kimeanzisha Mawkib (kituo cha huduma) cha kuwapokea wafanyaziyara, kikitoa chakula, vinywaji na vitafunwa, vikiwemo chupa 6,000 za maji, juisi 5,600 na peremende kila siku.
Aidha, kituo hicho kinaendesha vikao vya kila siku vya Qur’ani kando ya njia za wafanyaziyara, ikiwemo qiraa za Qur’ani kwa mtindo wa Kiraqi na wa Kimisri, shughuli shirikishi na wahifadhi wa Qur’ani, na vikao vya maombolezo vinavyoimarisha hali ya kiroho na kuwaelekeza zaidi mahujaji katika mafundisho ya Ahlul-Bayt (AS).
Shughuli hizi zinaonesha juhudi za Jukwaa la Kielimu la Qur’ani Tukufu katika kuwaunga mkono wafanyaziyara na kuandaa mazingira ya kina ya kiroho na kielimu kwa ajili ya ibada tukufu ya Arbaeen.
3494219