Hujjatul-Islam Hassan Shirzad, mtafiti katika Kituo cha Utamaduni na Maarifa ya Qur’ani, amesema kuwa “raslimali kubwa ya mwanadamu ni maisha yake,” akiongeza kuwa namna mtu anavyoyatumia ndiyo kipimo cha mafanikio ya kweli.
“Mfano bora kabisa ambaye Mwenyezi Mungu amemtambulisha kwa wanadamu ni Mtume Muhammad (SAW), ambaye tabia yake tukufu iliunganisha jamii iliyokuwa imegawanyika, na ambaye bado anaweza kuwaongoza Waislamu wa leo,” alisema Shirzad alipokuwa akihutubia mkutano wa ndani siku ya Jumapili.
Akinukuu Qur’ani Tukufu, alirejea aya ya 21 ya Surah al-Ahzab: "Hakika nyinyi mna mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu , kwa yule anayemtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na anayemkumbuka Mwenyezi Mungu sana." Alifafanua kuwa aya hii inaonesha kuwa kumfuata Mtume (SAW) kunahitaji imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu, imani ya Akhera, na dhikri ya mara kwa mara ya Mola.
Alinukuu pia maneno ya Imam Ali (AS) aliyesema: "Njia ya Mtume inakutosheni kama mfano wa kuigwa."
Kwa mujibu wa Shirzad, usafi wa moyo na uadilifu wa Mtume (SAW) unamfanya kuwa chanzo cha heshima kwa wanaomfuata, akibainisha: "Mtumishi mwenye heshima zaidi ni yule anayemfuata Mtume (SAW) na kutembea katika nyayo zake."
Shirzad alieleza kuwa Mtume Muhammad (SAW) aliongoza kwa muda wa miaka 23 na aliishi miongoni mwa watu kwa miaka 63. "Iwapo maadili, mwenendo na tabia zake zitazingatiwa kwa dhati, hususan na jamii za Kiislamu pamoja na viongozi wao, athari zake zitakuwa za kina," alisema.
Alinukuu pia aya ya 4 ya Surah Al-Qalam inayomwelezea Mtume (SAW): "Na hakika wewe una tabia njema kabisa."
Mtafiti huyo alisisitiza kuwa mwenendo wa kimaadili ni nguzo muhimu kwa mshikamano wa umma wa Kiislamu. Alinukuu maneno ya Mtume (SAW) aliyosema: "Wenye imani kamili zaidi miongoni mwa waumini ni wale wenye tabia njema," na "Wenye daraja bora zaidi katika imani ni wale wenye tabia njema."
Aliongeza kauli nyingine ya Mtume (SAW): "Waliokaribu zaidi nami Kesho katika Siku ya Kiyama ni wale wenye tabia njema."
"Mafundisho haya yanaonesha kuwa Mtume mkubwa wa Uislamu (SAW) ni mfano wa milele wa furaha, maadili na wokovu kwa wanadamu," alihitimisha Hujjatul Islam Shirzad.
3494298