IQNA

Misikiti duniani yahimizwa kuungana kulinda Al-Aqsa katika Siku ya Kimataifa ya Msikiti

23:19 - August 18, 2025
Habari ID: 3481103
IQNA – Mwanazuoni mmoja wa Kiirani amehimiza ushirikiano imara kati ya misikiti duniani, akisisitiza haja ya hatua za pamoja kulinda Msikiti wa Al-Aqsa dhidi ya uvamizi unaendelea wa utawala ghasibu wa Israel.

Hujjatul Islam Hojjatollah Zaker, mhadhiri wa  Hauza (vyuo vikuu vya Kiislamu) vyuo vikuu , vya kawaida amesema kwamba ukosefu wa uratibu wa kudumu kati ya misikiti katika ulimwengu wa Kiislamu umeufanya umma wa Kiislamu kushindwa kutoa majibu yenye nguvu kwa masuala muhimu, hasa hali ilivyo katika Msikiti wa Al-Aqsa.
 
“Uhusiano kati ya misikiti katika ulimwengu wa Kiislamu umekuwa wa muda mfupi tu. Ukosefu huu wa ushirikiano wa kudumu umezuia msimamo wa ulimwengu wa Kiislamu kuonekana kwa usahihi na kuwa na athari katika masuala kama Al-Aqsa,” alisema Hujjatul Islam Zaker katika mahojiano na IQNA kabla ya Siku ya Kimataifa ya Msikiti.
Kumbukumbu hii ya kila mwaka ilianzishwa kufuatia shambulio la moto dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa jijini Quds (Jerusalem) mnamo Agosti 1969, wakati mkazi Mzayuni alipoteketeza moto kwenye eneo hili takatifu, akiteketeza karibu mita za mraba 1,500 za jengo. Mnamo 2003, Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), kwa jitihada za Iran, lilitangaza rasmi Agosti 21 kama Siku ya a Kimataifa ya Msikiti ili kuhamasisha uelewa wa tishio linalokabili maeneo matakatifu ya Kiislamu hasa Al Aqsa.
 
Zaker alionya kwamba Al-Aqsa bado iko katika tishio linaloongezeka ambapo baadhi ya mawaziri wa mrengo wa kulia wa Israel na walowezi wa Kizayuni wakiendelea kuvamia eneo hilo takatifu la Waislamu.
 
Msikiti wa Al Aqsa uko katika eneo la Mashariki mwa Quds (Jerusalem), mji ambao unakaliwa kwa mabavu na utawala dhalimu wa Israel. Msikiti wa Al-Aqsa ni eneo la tatu kwa utakatifu katika Uislamu. Tangu uvamizi wa Israel dhidi ya eneo hilo mwaka 1967, eneo hili limekuwa chanzo cha mzozo mkubwa. Katika miaka ya karibuni, walowezi wa Kizayuni, wakilindwa na polis, waliingia  ndani ya Msikiti na kutekeleza ibada za Kiyahudi na hivyo kuvunja makubaliano ya muda mrefu kuhusu hali ya eneo. Uvamizi huu umechochea hasira miongoni mwa Wapalestina na kuvutia lawama kutoka sehemu mbalimbali za dunia ya Kiislamu.
 
Hujjatul Islam Zaker amewahimiza Waislamu kuchukua hatua madhubuti katika Siku ya Kimataifa ya Msikiti kwa kutoa khutuba maalumu, kueneza bendera za kuunga mkono Al-Aqsa, kufanya vikao vya Qur’ani, na kuandaa dua maalumu kwa ajili ya ukombozi wa al-Quds.
 
“Kila mtu katika ulimwengu wa Kiislamu anayejali Nyumba ya Mwenyezi Mungu lazima aendelee kupigania uhuru wa Al-Aqsa na al-Quds al-Sharif,” amesema.
 
Pia amesisitiza umuhimu wa kutumia zana za kisasa, hasa majukwaa ya kidijitali, katika kuhamasisha uungaji mkono harakati za ukombozi wa Al Aqsa. “Lazima tutumie mitandao ya kijamii kuelimisha jamii za Kiislamu kuhusu suala la Al-Aqsa. Tabaka zote za jamii zinapaswa kuonyesha wasiwasi wao, kuchukua msimamo, na kwa uwazi kusema hapana kwa utawala wa Kizionisti na ubaguzi wa kimataifa,” alisema.
 
Kiongozi huyo wa kidini amemaliza kwa kusema kwamba Siku ya Kimataifa ya Msikiti  inapaswa kuwa jukwaa la kuungana na kutoa msaada wa kimataifa kwa harakati za ukombozi waPalestina. “Ni fursa ya kuonyesha msaada wa kina kwa Al-Aqsa na Palestina kote duniani ya Kiislamu,” alibainisha.

3494301

Habari zinazohusiana
captcha