IQNA

Mtihani wa Kuwachagua Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Kufanyika Yemen

23:46 - August 06, 2025
Habari ID: 3481045
IQNA – Wizara ya Wakfu na Mwongozo ya Yemen imetangaza kuwa itafanya mtihani maalum kwa ajili ya kuwachagua wawakilishi wa nchi hiyo watakaoshiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika mataifa mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka cratar.net, wizara imesema kwamba mtihani huo unalenga kuwachagua wahifadhi bora wa Qur'ani Tukufu kutoka Yemen, watakaoiwakilisha nchi katika mashindano hayo ya kimataifa.

Aidha, imetangazwa kuwa muda wa usajili kwa ajili ya mtihani huo umeongezwa hadi mwisho wa mwezi wa Agosti.

Wizara imeeleza kuwa lengo la kuongeza muda wa usajili ni kutoa fursa zaidi kwa vijana wenye vipaji vya uhifadhi wa Qur'ani – wa kiume na wa kike – kujaribu uwezo wao wa kielimu na kiroho katika nyanja za Qur’ani.

Kulingana na tangazo hilo, mtihani huo utahusisha nyanja kuu tatu: kuhifadhi Qur’ani yote kwa ukamilifu, usomaji sahihi kwa Tajweed, na ustadi wa Qira’at kumi mashuhuri (aṣ-Ṣughra na al-Kubra).

Wizara imewataka maqarī na mahafidhina walioko tayari kushiriki na wanaotimiza masharti ya ushiriki, kufungua tovuti rasmi ya wizara na kujaza fomu maalum ya usajili iliyowekwa huko.

Mtihani huu ni sehemu ya sera za wizara zinazolenga kugundua na kukuza vipaji vya Qur’ani kutoka katika mikoa mbalimbali ya Yemen, pamoja na kuwaandaa kwa ajili ya uwakilishi wa heshima katika majukwaa ya kimataifa ya Qur’ani.

Wizara imesisitiza kuwa hatua hii pia inaonyesha nafasi ya Yemen katika harakati za Qur’ani na juhudi za kukuza elimu ya Dīn katika ngazi za kimataifa.

4298208

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu yemen
captcha