Tawi la wanawake la Chuo Kikuu cha Qur’ani na Sayansi Zake, mjini Sana’a, Yemen limeanza shughuli hizo chini ya kauli mbiu ya aya ya Qur’ani: “Lakini Mtume na wale walioamini pamoja naye walipigana kwa mali zao na nafsi zao. Hao watapata mema yote…” (Aya ya 88, Surah At-Tawbah).
Naibu Mkuu wa Chuo, Hanan al-Ezzi, amesisitiza maelekezo kutoka kwa Kiongozi Abdul Malik al-Houthi kuhusu umuhimu wa kutukuza hadhi ya Mtume Muhammad (SAW) miongoni mwa Waislamu, hususan Waislamu wa Yemen.
Wanafunzi Batoul al-Qadi na Ikhlas Aboud wameeleza umuhimu wa siku ya kuzaliwa kwa Mtume (SAW), inayojulikana kama Milad-un-Nabi, kama tukio lenye nafasi kubwa katika kuimarisha maadili mema na kuonesha mshikamano wa Yemen na Palestina kama jukumu la kidini na kibinadamu.
Wanafunzi hao wamesisitiza nafasi ya muda mrefu ya Wayemeni kama wafuasi waaminifu wa njia ya Mtume Muhammad (SAW), ambapo wananufaika na urithi wake wa subira na msimamo thabiti.
3494224