IQNA

Jinai za Israel

Vikosi vya Yemen kuendelea kushambulia meli yoyote inayofungamana na Israel

15:30 - May 17, 2024
Habari ID: 3478838
IQNA - Vikosi vya Yemen vitaendelea kulenga meli yoyote inayoelekea bandari zinazokaliwa kwa mabavu na Israel, bila kujali kama zinapitia Bahari ya Sham au la, kiongozi wa harakati ya Mapambano ya Kiislamu (muqawma)  ya Ansarullah alisema.

"Tutalenga meli yoyote inayoelekea Israel kwa kutumia anuwai ya silaha zetu," Abdul-Malik al-Houthi alisema katika hotuba ya televisheni siku ya Alhamisi.

Ansarullah na vikosi vingine vya Yemen ambavyo vimelenga meli zenye uhusiano na Israel katika Bahari ya Sham ili kuwaunga mkono Wapalestina, vimezidisha operesheni zao katika miezi ya hivi karibuni. Wameahidi kuendeleza mashambulio yao hadi pale Israel itakaposimamisha uvamizi wake katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa.

Kufikia sasa wiki hii, Ansarullah imefanya operesheni saba kwa makombora 13 ya balestiki katika Bahari Nyekundu, Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi, Houthi alisema Alhamisi.

"Hakuna mstari mwekundu kwetu. Tunapiga hatua kwa hatua malengo nyeti ya kimkakati ambayo yanamdhuru adui Mzayuni na tutawafikia kwa neema ya Mungu," alisema.

Al Houthi amesema Marekani inashirikiana na utawala wa Kizayuni katika mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Palestina, kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza na kufunga kivuko cha Rafah.

Amesema Wamarekani ndio waliouunga mkono utawala wa Israel katika kuanzisha hujuma  dhidi kivuko cha Rafah.

Kivuko cha Rafah kati ya Misri na kusini mwa Gaza kimekuwa njia muhimu ya misaada kwa eneo la Gaza, ambapo mgogoro wa kibinadamu umeongezeka na baadhi ya watu wako katika hatari ya njaa.

Mapema mwezi huu, majeshi ya Israel yalikalia kwa mabavu kivuko hicho kinachopakana na Misri katika kuandaa uvamizi wa ardhini katika mji wa Rafah ambapo mamia ya maelfu ya Wapalestina waliokimbia makazi yao wamekuwa wakipata hifadhi.

Ukaliaji huo umekuja baada ya Hamas kutangaza kuwa imekubali pendekezo la kusitisha mapigano kufuatia wiki kadhaa za mazungumzo na Qatar na Misri.

3488367

captcha