IQNA

Nakala 900,000 za Qur’ani kusambazwa miongoni mwa Mahujaji wanaoondoka Madina

13:21 - June 18, 2024
Habari ID: 3478979
IQNA - Zaidi ya nakala 900,000 za Qur'ani Tukufu zitakabidhiwa kama  zawadi kwa Mahujaji wanaoondoka Saudia kupitia viwanja vya ndege katika mji mtakatifu wa Madina mwaka huu. 

Osama Madkhali, mkurugenzi wa wizara ya masuala ya Kiislamu ya Saudia tawi la Madina, alisema maandalizi yanaendelea ili kuwasaidia Mahujaji wanaoondoka, hasa wale ambao huingia Madina na kuondoka kupitia viwanja vyake vya ndege.
Alisisitiza kwamba uratibu na Kiwanja cha Mfalme Fahd kwa ajili ya Uchapishaji wa Qur’ani Tukufu huko Madina umehakikisha ugawaji wa nakala zaidi ya 900,000 za Qur’ani Tukufu katika eneo hilo.
Nakala hizi zimehifadhiwa na kusambazwa katika maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Prince Mohammad bin Abdulaziz huko Madina na Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Prince Abdulmohsen bin Abdulaziz huko Yanbu, ambapo kumbi za kuondoka katika viwanja vyote viwili vya ndege zimetayarishwa kusaidia Mahujaji.
Wizara pia imekamilisha maandalizi yake ya kupokea kundi la kwanza la Mahujaji hasa wale wanaoondoka haraka baada ya kukamilisha ibada zao za Hijja.
Tawi la wizara hiyo huko Madina limetayarisha misikiti ya Al-Khandaq, Sayyid Al-Shuhada, na Qiblatain yenye mfumo jumuishi wa huduma kwa ajili ya kutembelewa na Mhujaji.
Mbali na kusambaza vitabu vya muongozo na uhamasishaji kwa Mahujaji wanaotembelea misikiti hiyo mikubwa, wizara imepanga ugawaji wa nakala za Quran Tukufu kwa Mahujaji wanaoondoka

 

 4222050

 

 

captcha