IQNA

Kadhia ya Palestina

Mashambulizi ya Israel kwenye Kambi ya Nuseirat yaua familia ya watu 17

10:06 - June 19, 2024
Habari ID: 3478984
Mashambulizi mawili tofauti ya vikosi vya Israeli kwenye kambi ya Nuseirat usiku wa kuamkia leo yaliwauwa watu wasiopungua 17 wa familia zilizokimbia makazi.

Shambulio la awali liliua watu kumi, miongoni mwao wakiwa ni wanawake na watoto, huku nusu ya majeruhi wakiwa wa familia moja, kulingana na ripoti zilizotolewa na  Al Jazeera.

Idadi ya waliojeruhiwa inaripotiwa kuwa mara mbili zaidi, na juhudi zinaendelea kuwaokoa wale ambao bado wamenasa chini ya vifusi.

Mashambulizi yaliyofuata, yalitokea saa moja tu baadaye na kuharibu nyumba ya familia nyingine, na kupoteza maisha ya wazazi, watoto wao,  babu na wazee.

 Kambi ya Nuseirat imeshuhudia mashambulizi ya kikatili ya Israel katika wiki zilizopita ya mara kwa mara Mapema mwezi huu, wanajeshi wa Israel waliwaua kwa umati Wapalestina wasiopungua 274 waliokimbia makazi yao katika operesheni ya kuwaachilia mateka wanne.

Al-Azhar imetoa ripoti kwamba: Ukatili wa Israel huko Ukanda wa Gaza ni aibu kwa Ubinadamu

Zaidi ya hayo, vifo viwili viliripotiwa kwenye barabara ya pwani katika eneo la kati-magharibi mwa Ukanda wa Gaza.

Na  Hospitali  hizo kwa sasa zinawahudumia takriban watu 35 walio na majeraha mabaya kutokana na mashambulizi hayo yaliyofanywa na utawala katili wa Israel huko Palestina Ukanda wa Gaza.

 Na kadhalika utawala huo haramu wa Israel umewaua zaidi ya Wapalestina 37,300,  na zaidi ya elfu 16,000 kati yao wakiwa watoto, tangu Oktoba 7 mwaka jana 2023.

 3488800

 

captcha