IQNA

Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) yakitayarisha kwa ajili ya Rakdha Tuwairaj

18:31 - July 15, 2024
Habari ID: 3479127
IQNA - Siku ya Ashura inapokaribia, Mfawidhi wa kaburi tukufu la Imam Hussein (AS) huko Karbala, Iraq, inajiandaa kwa ajili ya tukio la kila mwaka la Rakdha Tuwairaj.

Ali Fuad, afisa wa Idara ya  Mfawidhi wa kaburi (haram) tukufu la Imam Hussein (AS), alisema maeneo ya Haram takatifu yamefunikwa kwa mchanga ili kurahisisha harakati za wafanya ziyara wakati wa ibada. 

Kwa kuzingatia miongozo ya kiongozi mkuu wa Kishia wa Iraq Ayatollah Seyed Ali al-Sistani, idara hiyo imekusanya wafanyakazi wake wote na vifaa vya kuwahudumia wafanya ziyara wakati wa maombolezo ya siku za Muharram.

Muharram ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwandamo ya Hijri.

Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengineo katika sehemu mbali mbali za dunia hufanya maombolezao kila mwaka katika mwezi wa Muharram kuomboleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba zake.

Imamu wa tatu wa Shia (AS) na kikundi kidogo cha wafuasi wake na wanafamilia wake waliuawa kishahidi na dhalimu wa zama zake - Yazid Bin Muawiya, katika vita vya Karbala katika siku ya kumi ya Muharram (ijulikanayo kama Ashura) mwaka wa 61 Hijria Qamarai (680 Miladia)

Rakdha Tuwairaj ni tukio la siku ya Ashura ambapo waombolezaji hutembea bila viatu kutoka mji wa Hindya (zamani ukiitwa Tuwairaj) karibu na Karbala hadi kwenye haram tukufu ya Imam Hussein (AS) na Hazrat Abbas (AS) huku wakijipiga kichwa na kifua na kisha kuondoka na kisha kufanya ziyara .

Kituo cha Kiislamu cha Uingereza Huandaa  Maombolezo ya Muharram
Ni njia ya kufanya upya utii na matarajio ya mauaji ya siku za Ashura.

Ibada hiyo imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa takriban miaka 140, isipokuwa wakati utawala wa Baath wa dikteta wa zamani Saddam Hussein ukitawala Iraq.

 

3489119

 

captcha