Mamlaka ya Utangazaji ya Sharjah itakuwa ikianzisha chaneli ya Qur'ani chini ya maagizo ya Sultan bin Mohammed Al Qasimi, Mjumbe wa Baraza Kuu na Mtawala wa Sharjah, na ufuatiliaji wa Sultan bin Ahmed bin Sultan Al Qasimi, Naibu Mtawala wa Sharjah na Mwenyekiti wa Baraza la Habari la Sharjah.
Kauli mbiu ya TV ya Qur’ani ya Sharjah ni "Kuwa na Mungu na Mungu Atakuwa Pamoja Nawe.”
Kuanzishwa kwa Televisheni ya Qur'ani Tukufu ni sehemu ya mpango wa Mamlaka ya Utangazaji ya Sharjah kupanua mawasiliano yake ya habari na elimu.
Jukwaa hili jipya la vyombo vya habari lililoanzishwa na Mamlaka ya Utangazaji ya Sharjah limejitolea kwa ajili ya utangazaji endelevu wa Qur’ani Tukufu.
Salem Ali Al Ghaithi, Mkurugenzi wa SBA, alisisitiza uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa Mtawala wa Sharjah, kwa ajili ya uanzishwaji wa chaneli hii, akisisitiza umuhimu wa mradi huo na ulinganifu wake na uendelezaji wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu
Khalifa Hassan Khalaf, Mkurugenzi wa Idhaa ya Qur'ani Tukufu na Redio huko Sharjah amesema timu ya televisheni hiyo inayojumuisha watayarishaji na mafundi, ina wahitimu wa shahada za uzamili wa masomo ya Qur'ani, waliohifadhi Qur’ani , na wenye ijaza au idhini ya qiraa kumi. Timu hii ya wataalamu imejitolea kutayarisha vipindi ubora wa juu ili kutumiza matarajio ya watazamaji.
Chaneli hiyo itapatikana kwenye satelaiti ya Nilesat kwa mzunguko wa 11013H, kiwango cha alama 27500 V, QPSK ,sa 5/6. Inaweza pia kufikiwa kupitia Etisalat Live kwenye chaneli 579.
3489520