IQNA

Diplomasia

Afisa wa Uingereza ajiuzulu na kusema nchi yake ni mshirika wa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

17:26 - August 19, 2024
Habari ID: 3479303
IQNA-Mwanadiplomasia mwandamizi wa Uingereza amejiuzulu wadhifa wake katika Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo akipinga uuzaji silaha wa nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Mwanadiplomasia huyo amelaani hatua ya serikali ya London ya kuendelea kuiuzia Israel silaha na kuitaja kuwa haiwezi kutetewa.

Mark Smith amejiuzulu wadhifa wake kama Mkuu wa Idara ya Mipango ya Afrika, Utaalamu, Masuala ya Jumuiya ya Madola na Maendeleo katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza (FCDO). Smith ameandika barua yake ya kujiuzulu aliyoipa kichwa cha maneno: "Wizara ya Mambo ya Nje na Kushiriki Kwake katika Jinai za Kivita."

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Uingereza amejiuzulu wadhifa wake na kusema kwamba amechukua uamuzi wa kujiuzulu kazi yake ya muda mrefu katika uga wa diplomasia na kwamba hawezi kuendelea na kazi hiyo akifahamu kuwa idara hiyo inaweza kuwa imehusika katika jinai za kivita."

Uingereza, Marekani pamoja na Ujerumani na Italia ndio nchi kuu zinazouza silaha na zana za kijeshi kwa utawala wa Israel ambao hadi sasa umeuwa shahidi Wapalestina zaidi ya elfu 40 katika Ukanda wa Gaza tangu uanzishe mashambulizi na mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa ene hilo mwezi Oktoba mwaka jana. 

Mashinikizo yanaendelea kuikabili London ili isitishe mauzo ya silaha kwa Israel. Hata hivyo bado inaendelea kuupatia silaha utawala huo unaofanya mauaji dhidi ya watoto na wanawake huko Ukanda wa Gaza. 

3489554

captcha