IQNA

Waislamu Kenya

Hatimaye, Chuo Kikuu cha Nairobi kupata Msikiti

12:08 - October 15, 2024
Habari ID: 3479597
IQNA - Chuo Kikuu cha Nairobi hatimaye kitakuwa na msikiti mdogo kwenye kampasi kuu ya taasisi hiyo muhimu zaidi ya elimu nchini Kenya.

Msikiti huo ambao unajengwa zaidi ya nusu karne baada ya kuanzishwa rasmi chuo hicho utatumiwa na wanafunzi, wahadhiri na jamii ya Waislamu.
Chuo kikuu hicho chenye umri wa miaka 54 ni miongoni mwa vyuo vikuu bora zaidicha na msukumo wa kuanzishwa kwa msikiti huo ni wa zamani kama taasisi yenyewe.
Waislamu ndani ya chuo hicho wanasema kelele za kutaka msikiti huo zilianza mwaka wa 1972, miaka miwili baada ya chuo hicho kuwa chuo kikuu huru.
Siasa, tofauti kati ya makundi ya Kiislamu na wasiwasi wa utawala wa chuo kikuu juu ya umiliki, vyote vilizuia wasimamizi kuidhinisha msikiti hapo awali.
Lakini vizingiti viliondoka  mwaka jana ambapo  baada ya barua nyingi na majadiliano hatimaye utawala wa chuo uliidhinisha ujenzi wa msikiti wa muda kwenye eneo ambalo lilikuwa la maegesho ya gari lakini sasa halitumiki.
“Tuko katika harakati za kuujenga msikiti kwa msaada wa wanafunzi na jamii ya Kiislamu. Tunajarajiwa kukamilisha mradi kabla ya Desemba," Sheikh Muhammad Abdallah, mhubiri wa Kiislamu katika chuo kikuu hicho, amesema katika mahojiano na RNS. "Mafanikio hayo yanamaanisha mengi ... Kutakuwa na uttulivu unaohitajika wakati wa kuwasiliana na Mwenyezi Mungu."
Kulingana na mhubiri huyo wa Kiislamu, idadi ya wanafunzi Waislamu katika chuo kikuu imekuwa ikiongezeka - na msikiti huo mpya utasaidia kuhudumia jamii hiyo.
Msikiti huo utajengwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kupunguza gharama kadiri itakavyowezekana. Sheikh Abdallah alisema mradi huo utagharimu kati ya dola 47,000 na 67,000 (shilingi milioni 6-8 za Kenya), ikijumuisha mazulia ya swala na vipaza sauti.
Katika kikao kimoja, msikiti huo utachukua takriban watu 300, na hivyo ni msikiti mdogo, alisema Dakta Sheikh Hassan Kinyua Omari, mwanazuoni wa kidini katika chuo kikuu hicho.
"Nairobi ndicho chuo kikuu kinachoongoza Afrika Mashariki, na nadhani hili litakuwa somo kubwa kwa vyuo vikuu vyote vya nchi hii kwamba lazima tupe heshima sawa kwa dini zote," alisema na kuongeza kuwa kujenga msikiti kwenye chuo kikuu kutafanya Chuo Kikuu cha Nairobi kiwe neme ya maelewano ya kidini. Dakta Omari amesema tayari kuna kanisa na ukumbi wa ibada kwa wote katika chuo hicho.
Wanafunzi Waislamu kwa sasa wanaswali kwenye nafasi nyuma ya maktaba kuu, ambapo mara nyingi wanakabiliwa na usumbufu kutokana na kuwa ni kando ya njia ya miguu.
"Umeona hali mbaya ya mahali tunaposwali," alisema Mohammed Abdul Sheemaka, mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Nairobi. "Ni bahati umekuja hapa wakati hakuna mvua, lakini wakati wa mvua, kungekuwa na matope na mvua huvuja sana; huwezi kuswali katika eneo hilo.”
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa wanafunzi, Waislamu katika chuo hicho na kampasi jirani, wakiwemo wanafunzi wa zamani, wanasherehekea msikiti huo mpya.
"Watu waliposikia kwamba hatimaye chuo kikuu kimetutengea ardhi, kila mtu ... alimshukuru Mungu ... kwa sababu haya ni mapambano ambayo yamekuwa hapa kwa muda mrefu," amesema.
Kiongozi huyo wa wanafunzi amesema msikiti huo umechelewa kujengwa kwa vile vyuo vikuu vingine vya Afrika Mashariki, kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, vina misikiti.
"Tumekuwa tukiuliza, 'Kwa nini sio Chuo Kikuu cha Nairobi?'" alisema.
Utakapojengwa hatimaye, Msikiti huo utasimama mita chache kutoka Kanisa la Chuo Kikuu la St Paul na Kanisa Kuu la St Andrew's Presbyterian na Kanisha la Uhuru Highway Lutheran kati ya maeneo mengine ya maeneo ya ibada ya Kikristo..
Sheikh Kinyua amesema makasisi watatu Wakristo  katika chuo kikuu wameunga mkono msikiti huo.
"Sioni upinzani wowote, lakini ukitokea, hilo ni suala la utawala wa chuo," alisema.
Kasisi Hosea Kiprono Mitei, kasisi wa Kiprotestanti katika chuo kikuu hicho, alithibitisha kwamba msikiti huo haupingwe na yeyote miongoni mwa Wakristo kwa vile wengine wote wana nafasi za ibada.
"Wanafunzi wa Kiislamu hawana mahali pazuri pa kuswali. Aidha hiki sio chuo cha Kikristo. Sidhani kama kutakuwa na upinzani wowote,” alisema.
Sheikh Abdallah anatumai kuwa msikiti unaweza kuwa mahali ambapo, mbali na swala za kila siku na Ijumaa, wanafunzi wanaweza kupata utulivu na mahali pa kupumzika, kusoma Qur'ani au mazungumzo kati yao. Viongozi wa Kiislamu wanaweza pia kutembelea msikiti ili kutoa hotuba ili kuinua hali ya kiroho ya wanafunzi.
"Watu waliposikia kwamba hatimaye chuo kikuu kimetupatia ardhi, kila mtu ... alimshukuru Mwenyezi Mungu ... kwa sababu haya ni mapambano ambayo yamekuwa hapa kwa muda mrefu," alisema.
 

3490245

Kishikizo: nairobi msikiti
captcha