IQNA

Usomaji wa Qur'ani katika duka la sandwichi New York waaenea mitandao ya kijamii

14:15 - October 17, 2024
Habari ID: 3479606
IQNA - Video ya mtu akisoma Qur'ani Tukufu katika duka la sandwichi katika mtaa wa Times Square mjini New York City licha ya kutozwa faini ya $50 imevutia watu wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Klipu iliyosambazwa na mtalii wa Kituruki huko New York imesambaa. Video hiyo inamuonyesha mmiliki wa mkahawa mdogo ambaye anarusha hewani visomo vya Qur'ani Tukufu kila siku, licha ya kutozwa faini.

Alipoulizwa na mtalii huyo wa Kituruki jinsi anavyoweza kurusha hewani qiraa Qur'ani kwa sauti kubwa na ikiwa ni jambo hilo linaidhinishwa kisheria, mmiliki wa mgahawa alieleza kuwa amekubali kulipa faini ya dola 50 kila siku ili aendelee kurusha hewani qiraa hiyo ya Qur'ani Tukufu.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wamepongeza hatua ya mhamiaji huyu wa Misri, ambaye anauza sandwichi na juisi kutoka kwenye duka lake dogo katikati mwa Jiji la New York.

4242343

captcha