IQNA

Maqari mashuhuri wa Iran kushiriki kikao cha Qur'ani Katika Msikiti wa Istiqlal, Indonesia

12:58 - March 14, 2025
Habari ID: 3480370
IQNA – Maqari maarufu wa Qur'ani kutoka Iran, Hamed Shakernejad na Ahmad Abolqassemi, wanatarajiwa kushiriki katika moja ya vikao vikubwa zaidi vya Qur'ani Tukufu katika Msikiti mashuhuri wa Istiqlal, Indonesia.

Tukio hili limepangwa kufanyika Machi 16 na litawaleta pamoja viongozi mashuhuri kutoka nchi za Kusini Mashariki mwa Asia huku likikuza maingiliano ya kitamaduni baina ya dini mbalimbali.

Mpango huu umeandaliwa kwa ushirikiano wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano la Kiislamu la Iran, Mwambata Kiutamaduni wa Ubalozi wa Iran nchini Indonesia, na kipindi cha televisheni cha Mahfel.

Mahfel, maarufu kwa kuonesha usomaji wa Quran na kueneza mafundisho ya Kiislamu, ni mfululizo wa vipindi vya televisheni vya Iran vinavyopendwa na watazamaji duniani kote.

Wageni mashuhuri, wakiwemo Waziri wa Masuala ya Kidini wa Indonesia na Profesa Nasaruddin Umar, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Istiqlal, wanatarajiwa kuhudhuria.

Inaripotiwa kuwa juhudi zinaendelea kufanywa ili kuratibu uwepo wa Rais wa Indonesia, Prabowo Subianto, kwenye hafla hiyo.

Mkusanyiko huo wa Qur'ani utapeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni na YouTube.

Zaidi ya hayo, Mwambata wa Kitamaduni wa Iran ameandaa pia programu za ziada za Qur'ani katika vituo vingine kadhaa nchini Indonesia, ikiwa ni pamoja na Msikiti wa Al-Azhar na Pesantren Al-Qur’aniyah.

Prominent Iranian Qaris to Lead Quranic Program at Indonesia's Istiqlal Mosque

3492318

 

Habari zinazohusiana
captcha