IQNA

Kufa Shahidi Katika Qur'ani/1

Hadhi ya Juu ya Kufa Shahidi Katika Uislamu

17:45 - November 20, 2024
Habari ID: 3479782
IQNA – Qur’ani Tukufu inasisitiza kwamba kifo cha kishahidi ni hadhi iliyotukuka na inaorodhesha fadhila nyingi kwa mashahidi.

Mojawapo ya sifa hizo ni kwamba mashahidi hupata baraka tele za Mwenyezi Mungu na wanafurahia sana jambo hilo.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 170 ya Suratul Imran: “Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika."

Kulingana na aya hii, mashahidi wako hai kweli kwa sababu wana ushawishi mkubwa katika ulimwengu huu na wanaweza kuwasaidia ndugu zao katika imani.

Wanawapa ndugu zao habari njema kwa imani kwamba hawapaswi kuwa na woga au wasiwasi. Ni kwa sababu mashahidi wanaona hadhi na malipo ya ndugu zao.

Pia kuna Hadith za kinabii zinazosisitiza umuhimu na hadhi ya kifo cha kishahidi. Mtukufu Mtume (SAW) amesema: “Kwa kila wema kuna bora zaidi isipokuwa kufa kishahidi, kwa sababu mtu anapokufa kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, hakuna wema zaidi ya huo."

Mtume (SAW) pia amesema makundi matatu ya watu yatawaombea wengine shifaa siku ya Qiyama: Mitume, kisha wanachuoni, kisha mashahidi.

Imam Ali (AS), kama sahaba wa Mtukufu Mtume (SAW), anasema kuhusu kifo cha kishahidi: “Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mkononi mwake, mapigo elfu moja kwa upanga hakika ni mepesi zaidi [kwangu] kuliko kufa kitandani."

Wale waliouawa kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, sio tu kwamba wataingia peponi bali pia Mwenyezi Mungu hulipa thawabu zao na matendo yao duniani:

….Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a´mali zao. Atawaongoza na awatengezee hali yao. Na atawaingiza katika Pepo aliyo wajuulisha.” (Aya 4-6 za Sura Muhammad)

3490667

Kishikizo: qurani tukufu shahidi
captcha