IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Shahidi Hassan Nasrallah alikuwa na nafasi muhimu kuimarisha mshikamano wa Waislamu

20:33 - February 21, 2025
Habari ID: 3480250
IQNA-Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amezungumzia mazishi yajayo ya shahidi Sayyid Hassan Nasrallah na kusema: alikuwa mtu mwenye heshima na aliuletea umma wa Kiislamu heshima. Alikuwa shakhsia mashuhuri ambaye alikuwa nafasi muhimu katika kuondoa migogoro na kuimarisha mshikamano katika umma wa Kiislamu

te

Hujjatul Islam Abutorabi-Fard ameendelea kusisitiza kuwa: "Tuko katika hatua ya mwisho ya mazishi yenye heshima na yenye kuleta nguvu ya kiongozi wa muqawama, kamanda shujaa, mwanazuoni na mtu madhubuti wa Hizbullah. Shakhsia huyu alikuwa bega imara la mapinduzi na umma, pamoja na mhimili wa muqawama, akiwa na sifa za kipekee. Sifa ambazo Kiongozi Muadhamu anasema kuwa kweli  zimeuletea Uislamu heshima. Heshima hii ni matunda ya imani na matendo mema aliyoyafanya. Alikuwa mtu mwenye heshima na mjumbe wa heshima kwa umma wa Kiislamu."

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo Tehran ameendelea kusema: "Shahidi Nasrallah alikuwa mtu mwenye busara na asiye na kifani ambaye kwa miongo kadhaa aliongoza muqawama na Hizbullah, akifungua njia ya kuunda nguvu nyingine katika ulimwengu wa Kiislamu na pia kuunganisha safu za mhimili wa muqawama. Leo, tunashuhudia nguvu ya muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon, uimara wa Yemen, ushindi wa wapiganaji wa Gaza na msimamo thabiti wa wanamuqawama wa ulimwengu wa Kiislamu."

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeandaa mazishi ya Sayyid Hassan Nasrallah na mkuu wa Halmashauri Kuu yake, Sayed Hashem Safieddine, mnamo Februari 23.

Nasrallah aliuawa shahidi katika shambulizi kubwa la anga la Israel huko Beirut mnamo Septemba 2024. Safieddine pia aliuawa shahidi katika shambulio la Israel mnamo Oktoba.

4267402

Habari zinazohusiana
captcha