IQNA

Maonyesho na semina za mafunzo  zimepangwa pembeni mwa mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu  nchini  Indonesia

17:15 - January 30, 2025
Habari ID: 3480129
IQNA - Mashindano ya 4 ya Kimataifa ya usomaji wa Qur’ani Tukufu  ya Indonesia, au Musabaqah Tilawatil Qur’an (MTQ), pia yanajumuisha mijadala, maonyesho, na Semina za mafunzo.

Mashindano ya 4 ya Kimataifa ya Usomaji wa Qura’ni ya Indonesia yawaleta pamoja washiriki 60 kutoka Mataifa 38

Washiriki sitini (60) kutoka mataifa 38 barani Asia, Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, na Marekani wamejiunga na mashindano haya mwaka huu.

Mashindano haya yalianza Jakarta tarehe 28 Januari na yataendelea hadi tarehe 2 Februari 2025.

"Tumekuwa tukizingatia kuandaa mashindano ya kitaifa ya MTQ, lakini sasa tunaanza kuandaa mashindano ya kiwango cha kimataifa," alisema Waziri wa Mambo ya Kidini wa Indonesia, Nasaruddin Umar, wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo jijini Jakarta siku ya Jumatano.

Alisisitiza kuwa, watu kutoka kote ulimwenguni wameonyesha hamasa kubwa ya kushiriki mashindano haya, akibainisha kuwa washiriki kutoka mataifa 187 walishiriki katika hatua ya awali ya kufuzu mtandaoni mwaka 2023.

Miongoni mwa washiriki 60 waliostahili kufika hatua ya nusu fainali huko Jakarta, wapo washindani kutoka Uholanzi, Russia, Sweden, Italia, na Canada.

Nchi kadhaa za Afrika, zikiwemo Misri, Libya, Tanzania, Mauritania, Guinea, Kenya, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nigeria, Ivory Coast, Ghana, Somalia, Chad, Cameroon, Burkina Faso, Guinea-Bissau, na Msumbiji, pia zimetuma wawakilishi wao.

Zaidi ya hayo, washiriki kutoka Indonesia, Malaysia, Brunei Darussalam, Thailand, Singapore, Ufilipino, Iran, Syria, Pakistan, Afghanistan, India, Bangladesh, Kuwait, Uturuki, Yemen, na Palestina pia wanashiriki mashindano haya.

Zaidi ya usomaji wa Qur’ani

Waziri Umar alifafanua kuwa, pamoja na mashindano ya usomaji wa Qur’ani, tukio hilo pia linajumuisha:

Mashindano ya wahifdhi wa  Qur’ani Tukufu 

Mijadala,

Maonyesho, na

Warsha za elimu.

"Pia tunatoa shughuli za utangulizi wa tamaduni na matembezi ya mji, kwa kuzingatia kuwa washiriki wetu ni wageni kutoka mataifa mengine, wengi wao huenda hawajawahi kutembelea Indonesia hapo awali. Tutawaongoza kwenye maeneo maalum yenye kuvutia," alieleza.

Mashindano ya kimataifa ya MTQ mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu:

"Qur’ani, Mazingira, na Ubinadamu kwa Maelewano ya Ulimwengu."

"Kaulimbiu hii inatuhimiza kuthibitisha kuwa Qur’ani Tukufu  ni moja ya vitabu tukufu  vinavyozingatia kwa kina umuhimu wa utunzaji wa mazingira," aliongeza hayo katka maongezi yake.

 

 

 

https://iqna.ir/en/news/3491663/

captcha