IQNA

Mashindano ya 29 ya Qur’ani Tukufu ya huko  Bahrain yaanza kwa ushiriki wa zaidi ya watu 4,200

14:48 - February 03, 2025
Habari ID: 3480154
IQNA – Toleo la 29 la mashindano Makuu ya Qur’ani Tukufu ya Bahrain lilianza rasmi siku ya Jumamosi katika Kituo cha Kiislamu cha Al Fateh.

Mashindano haya yanaandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Haki, Masuala ya Kiislamu na Wakfu pamoja na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Bahrain (BNA), jumla ya washiriki 4,242 wamejiandikisha, huku 703 kati yao wakiendelea kwenye hatua za awali. 

Kwa mujibu wa Abdulla Al Omari, Mkurugenzi wa Masuala ya Qur’ani katika wizara hiyo, mashindano yanapitia hatua kadhaa, kuanzia mashindano ya awali ya ndani hadi kufikia hatua ya fainali.

Mashindano haya yanajumuisha makundi saba, yanayoshughulikia hifdhi (uhifadhi wa Qur’ani) na usomaji (qiraa). Pia kuna mashindano maalum kwa wanafunzi wa shule, watu wenye ulemavu, wafungwa, wasemaji wa lugha zisizo za Kiarabu, na wananchi kwa ujumla.

Mbali na mashindano makuu, tuzo za nyongeza zinatolewa kwa mafanikio mbalimbali, zikiwemo tuzo kwa mshiriki mdogo zaidi na mzee zaidi, kituo Bora cha Qur’ani, na mashindano bora ya ndani ya nchi.

 

 3491708

 

 

 

Kishikizo: qur'ani hatua wanafunzi
captcha