IQNA

Kiongozi Muadhamu asifu Tafsiri ya Tasnim Kama Chanzo cha Fahari kwa vyuo vya Kiislamu

19:37 - February 24, 2025
Habari ID: 3480262
IQNA – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemsifu Ayatullah Abdollah Javadi Amoli kwa mchango wake wa miongo kadhaa katika tafsiri ya Qur’ani, akielezea Tafsiri yake ya Tasnim kama mafanikio makubwa ya kielimu kwa vyuo vikuu vya Kiislamu au Huzah.

Kauli za Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, alizozitoa wakati wa mkutano na waandalizi wa Mkutano wa Kimataifa wa Tafsir Tasnim mnamo Februari 22, 2025, zilitangazwa hadharani leo katika mkutano uliofanyika mjini Qom, ukiashiria kukamilika kwa tafsiri hiyo.

Ayatullah Khamenei alimpongeza Ayatullah Javadi Amoli kwa juhudi zake katika tafsiri ya Qur’ani, akibainisha kuwa utafiti, ufundishaji, na uandishi wake kwa zaidi ya miaka 40 vimeacha athari kubwa katika elimu ya Kiislamu.

"Hauzah ina deni kubwa kwa juhudi zake za kukusanya na kufundisha Tafsir Tasnim," alisema.

Aidha, alitambua mchango wa Ayatullah Javadi Amoli katika sayansi ya mantiki, pamoja na fiqhi, falsafa, na tasawwuf. Hata hivyo, alisisitiza kuwa "hakuna kati ya haya yanayoweza kulinganishwa na kazi yake ya tafsiri ya Qur’ani."

Kiongozi huyo alielezea Tafsir Tasnim kama “chanzo cha fahari” kwa utafiti wa Kishia na seminari za Kiislamu.

"Mtazamo wa kiakili wa mfasiri umechangia sana katika kufafanua maana za kina zilizomo ndani ya aya za Qur’ani," alisema.

Akilinganisha kazi hiyo na Tafsir al-Mizan ya Allamah Tabatabai, Ayatullah Khamenei alibainisha kuwa Tafsir Tasnim ina wigo mpana zaidi na inatoa mtazamo wa kisasa zaidi, hivyo kuifanya kuwa rejea ya kiensiklopedikia kwa wanazuoni na wanafunzi.

Pia alisisitiza umuhimu wa kuandaa faharasa ya kiufundi na kimaudhui ili kurahisisha ufikivu wa kazi hiyo pana.

Akielezea wasiwasi wake kuhusu umakini mdogo wa seminari katika tafsiri ya Qur’ani, alimtukuza marehemu Allameh Tabatabai kama mwanzilishi wa tafsiri za kisasa za Qur’ani.

Alikaribisha ongezeko la kozi za tafsiri ya Qur’ani mjini Qom, akisema, “Jambo la kuwa na takriban vikao 200 vya tafsiri katika seminari ya Qom ni maendeleo mazuri yanayopaswa kuimarishwa na kuendelezwa.”

Zaidi ya hayo, Ayatullah Khamenei alisisitiza umuhimu wa kukamilisha tafsiri ya Kiarabu ya Tafsir Tasnim ili kuifanya ipatikane kwa urahisi zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu.

Alitoa pia shukrani zake kwa Ayatullah Javadi Amoli na timu ya wanazuoni waliokuwa wakihusika katika kuandaa kazi hiyo.

Mwanzoni mwa mkutano huo, Ayatollah Alireza Arafi, mkuu wa seminari za Iran, alitoa muhtasari wa mkutano huo na kueleza mbinu za kipekee za kimaudhui na taaluma mbalimbali zilizotumiwa katika Tafsir Tasnim.

Hujatul Islam Saeed Javadi Amoli, mkuu wa Taasisi ya Isra, pia alizungumza katika hafla hiyo, akielezea mbinu ya uandishi na uundaji wa Tafsir ya Tasnim na juhudi za utafiti wa pamoja zilizopelekea maendeleo yake.

Alifikisha pia salamu za Ayatullah Javadi Amoli kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Tafsir Tasnim, iliyoandikwa na Ayatullah Javadi Amoli, ina juzuu 80 na ni matokeo ya zaidi ya miongo minne ya juhudi za kielimu.

Kazi hiyo inafuata mbinu ya tafsiri ya “Qur’ani kwa Qur’ani,” ikichambua aya teule kwa hatua nne.

3492007

Kishikizo: Tafsiri ya Qurani
captcha