Hujjatul Islam Morteza Javadi Amoli, mtoto wa mwanazuoni huyo mashuhuri, amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Qum Jumamosi kwamba sherehe hiyo, iliyopangwa Februari 20, 2025, itahutubiwa na Ayatullah Ali Reza Aarafi, mwenyekiti wa Vyuo vya Kiislamu (Hauza) nchini Iran.
Amesema sherehe kama hizo pia zitafanyika katika nchi zingine kadhaa.
Alibainisha kwamba tafsiri hiyo ambayo imepewa jina la Tafsiri ya Tasnim ya Qur’ani Tukufu imechapishwa katika jildi 80, na ni matokeo ya darsa za tafsiri za Ayatullah Javadi Amoli katika kipindi cha zaidi ya miaka 40.
Tafsiri hiyo inahusu masuala yote ya tafsiri ya Qur'ani yaliyojadiliwa na wanazuoni madhehebu za Kiislamu za Shia na Sunni, alisema.
Ayatullah Javadi Amoli amefasiri Qur’ani Tukufu kwa kutegemea Hadith kwa muelekeo wa kifalsafa, kimaadili, kitheolojia, … ili iweze kunufaisha jamii ya wasomi na watafiti wa sayansi za jamii, aliongeza.
Hujjatul Islam Javadi Amoli, ambaye anaongoza Wakfu wa Kimataifa wa Isra wa Sayansi ya Wahy, alisema zaidi kuwa Idara ya Tafsiri ya Qur’ani ya Tasnim itaanzishwa ili watafiti na wasomi watatoa majibu ya maswali na maoni kuhusu tafsiri ya Qur'ani.
Tafsiri ya Tasnim wa Qur’ani Tukufu imetajwa kuwa tafsiri ya kina zaidi ya Qur’ani katika historia ya Uislamu.
Jina lake linatokana na aya ya 27 na 28 za Surah Al-Mutaffifin: “Na mchanganyiko wake ni maji ya Tasnim. Ni chemchemi ambayo kwayo wanakunywa wale waliokaribishwa (kwa Mwenyezi Mungu).
Vikao hivyo vya tafsiri ya Qur’ani vya Ayatullah Javadi Amoli vilianza mnamo 1980 na kukamilika Aprili 2020.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Ulimwengu wa Kiislamu (ISESCO) liliitangaza tafsrii hiyo mnamo 2006 kama "Kazi ya Juu ya Utafiti katika Uga wa Mafunzo ya Kiislamu na Qur’ani".
3491053