IQNA

Masharti ya Trump ya ‘Israel Kwanza’ kwa Misaada ya Maafa ni Shambulio Dhidi ya Uhuru wa Maoni na Haki za Binadamu – CAIR

0:03 - August 07, 2025
Habari ID: 3481048
IQNA – Shirika moja la utetezi wa haki limeshutumu agizo jipya kutoka kwa serikali ya Trump linalozuia utoaji wa misaada ya majanga kwa majimbo na miji ya Marekani inayopinga bidhaa na makampuni ya Israel yanayoshiriki katika uhalifu wa kivita, likilitaja kuwa si la kizalendo, linakiuka katiba, na ni shambulio dhidi ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.

Baraza la Mahusiano ya Waislamu wa Marekani (CAIR) , shirika kubwa zaidi la haki za kiraia na utetezi wa Waislamu nchini Marekani siku ya Jumatatu liliitaja sera hiyo kuwa ni shambulio jipya la "Israel Kwanza" dhidi ya uhuru wa kujieleza na haki za binadamu, ambalo linahatarisha maisha ya Wamarekani wakati wa majanga ya baadaye ili kulinda utawala wa kigeni unaotekeleza mauaji ya halaiki na ubaguzi wa rangi.

Kwa mujibu wa Shirika la Usimamizi wa Dharura la Marekani (FEMA), sasa majimbo yanapaswa kufuata "masharti mapya" yanayowataka yasikate uhusiano wa kibiashara hasa na makampuni ya Kizayuni ya Kiyahudi ili kupewa msaada wa majanga.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi wa Masuala ya Serikali wa CAIR, Robert McCaw, alisema:

"Hitaji la utawala wa Trump kwamba miji na majimbo ya Marekani yanayokumbwa na maafa ya kiasili yasusie kampuni za Kizayuni zinazoshiriki katika uhalifu wa kivita ili yaweze kupokea msaada wa serikali ni jambo linalokiuka waziwazi katiba ya Marekani na halina utu."

"Ni jambo la ajabu na lisilo na mantiki: kwa mujibu wa kanuni mpya, majimbo na miji ya Marekani yanaweza kususia nchi yoyote duniani kwa sababu ya ukiukaji wa haki za binadamu – hata Marekani yenyewe – lakini si Israel. Hii si sera ya 'America Kwanza'. Hii ni sera ya 'Israel Kwanza' na haifai kuendelezwa."

"Sera hii ya kushtua inadhihirisha tena kuwa utawala wa Trump umetekwa na wafuasi wa siasa kali za Israel Kwanza, ambao wako tayari kuhatarisha maisha ya Wamarekani, kuzuia uhuru wa kikatiba, na kuruhusu mauaji ya halaiki ili kuipendezesha serikali ya kigeni inayoongozwa na mtuhumiwa wa uhalifu wa kivita. Kuweka masharti ya msaada wa kuokoa maisha juu ya utii wa kisiasa kwa utawala wa kivita ni ukatili, na ni ishara ya udikteta."

"Haki ya kususia (boycott) ni mojawapo ya uhuru wa msingi wa Katiba ya Marekani kupitia Marekebisho ya Kwanza (First Amendment). Kunyima misaada ya dharura kwa miji na majimbo yanayopigania haki za binadamu kunaweza kusababisha vifo wakati wa majanga kama vile vimbunga, mafuriko, na moto wa nyika. Hii ni sera ya ukatili wa serikali, inayoharibu demokrasia ya ndani huku ikiunga mkono mauaji ya halaiki na ubaguzi wa rangi huko nje.

/3494142/t

Kishikizo: donald trump israel vita
captcha