IQNA – Muungano wa Walimu wa Marekani (American Federation of Teachers - AFT) umeitupia lawama utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kusababisha mgogoro wa walimu katika ardhi za Palestina, huku ukitoa wito wa kukomeshwa kwa uchokozi dhidi ya Lebanon na kuondolewa kwa mzingiro haramu uliowekwa kwenye bandari za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3482520 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/21
IQNA-Iran imeonya kwamba italenga kila miundombinu iliyosalia katika eneo hili iwapo miundombinu yake itashambuliwa.
Habari ID: 3482494 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/16
IQNA – Vatikani (Vatican) imekataa jaribio la balozi wa utawala wa Trump katika Vatikan la kuwasilisha ukosoaji wa Papa Leo wa XIV dhidi ya vita vya Marekani dhidi ya Iran kana kwamba ulikuwa uingiliaji wa kisiasa badala ya msimamo wa kidini.
Habari ID: 3482484 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/14
IQNA-Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza rasmi kuwa, katika hatua ya kwanza ya kujibu uchokozi wa Marekani wa usiku wa kuamkia leo, vikosi vya wanamaji na anga vya Jeshi hilo, katika operesheni ya pamoja ya makombora na ndege zisizo na rubani (drones), vimetekeleza kwa mafanikio mashambulizi makali dhidi ya shabaha 85 muhimu vya kijeshi la Marekani na kutungua ndege moja ya kisasa ya kijasusi ya adui aina ya MQ9.
Habari ID: 3482458 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/08
IQNA-Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limeendesha oparesheni kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani (droni) dhidi ya vituo nane vya kijeshi vya Marekani katika kanda hii, likiitaja hatua hiyo kuwa “jibu madhubuti” dhidi ya uchokozi mpya wa Marekani kwenye ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3482414 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/28
IQNA-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Mkataba wa Maelewano (MoU) wa kumaliza vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran haukuwa matokeo ya shinikizo au kulazimishwa, bali ni zao la ustahimilivu na nguvu ya taifa shupavu la Iran.
Habari ID: 3482399 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/24
IQNA-Rais wa Iran ametoa wito wa ushirikiano wa karibu zaidi miongoni mwa nchi za Kiislamu, akisema Iran imenyoosha “mkono wa urafiki” kwa nchi za kanda hii katika harakati za kutafuta mfumo mpya wa usalama.
Habari ID: 3482398 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/24
IQNA – Maombolezo ya Muharram kwa ajili ya Imam Hussein (AS) yamefanyika karibu na Husseiniyeh ya Imam Khomeini (RA) jijini Tehran, siku ya Jumapili jioni.
Habari ID: 3482391 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/22
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, amesema maafisa wa Iran wamefanya juhudi kubwa kwa nia njema na kwa kujali maslahi ya taifa ili kufikia hati ya makubaliano (MoU) na Marekani, huku rais wa Marekani akitumia mbinu mbalimbali kutokana na hali ya kukata tamaa.
Habari ID: 3482379 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/19
IQNA-Hati ya makubaliano (MoU) kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani sasa imetiwa saini rasmi na marais wa nchi hizo mbili baada ya maandishi yake kukamilishwa, na hivyo makubaliano hayo kuanza kutekelezwa. Hayo yametangazwa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Jumatano usiku.
Habari ID: 3482374 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/18
IQNA – Hati ya makubaliano (MoU) kati ya Iran na Marekani imepongezwa na Papa Leo XIV, ambaye ameielezea kuwa hatua muhimu ya kujiepusha na vita.
Habari ID: 3482371 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/17
IQNA-Sekretarieti ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC) imethibitisha kuwa Iran na Marekani zimekamilisha maandishi ya hati ya makubaliano (MoU) yanayolenga kumaliza vita, kusimamisha mara moja na kwa kudumu operesheni zote za kijeshi katika nyanja zote, ikiwemo Lebanon, na pia kuondoa mzingiro wa baharini uliowekwa na Marekani dhidi ya Iran.
Habari ID: 3482361 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/15
IQNA-Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) likishirikiana na Jeshi la Kitaifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (Artesh), limetangaza mfululizo wa operesheni za kijeshi za kulipiza kisasi zilizoratibiwa vyema dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3482349 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/11
IQNA – Katika kauli yenye ukali dhidi ya sera za Rais wa Marekani Donald Trump, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema kwamba vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran havina uhalali wa maadili.
Habari ID: 3482334 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/07
IQNA-Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limeshambulia kambi mbili za anga za Marekani huko Kuwait na vituo vilivyobaki vya Kikosi cha Tano cha Jeshi la Wanamaji la Marekani (US Fifth Fleet) huko Bahrain ili kujibu uchokozi wa hivi karibuni wa Marekani.
Habari ID: 3482327 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/06
IQNA – Mstahiki Meya wa Jiji la New York, Zohran Mamdani, amelaani vikali vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran akivitaja kuwa ni mgogoro usio na msingi, na kusisitiza kuwa vita hivyo ni lazima viishe mara moja kwa ajili ya usalama wa raia wa mataifa mengine, na pia kwa manufaa ya Wamarekani wanaopambana na hali ngumu ya maisha nyumbani kwao.
Habari ID: 3482297 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/29
IQNA – Rais wa Iran Masoud Pezeshkian katika ujumbe wake kwa Papa Leo XIV ameshukuru misimamo ya kimaadili ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, akiyataja kuwa ni ukiukaji wa utawala wa sheria na wa maadili ya kibinadamu.
Habari ID: 3482246 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/16
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa
IQNA-Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa kimesema kuwa ushiriki, uwezeshaji na ushirikiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika vita vya hivi karibuni vya uchokozi vilivyoanzishwa na Marekani pamoja na utawala wa Israel dhidi ya Iran ni sawa na “kusaidia kambi ya ukafiri dhidi ya ndugu Waislamu” na kwa hivyo ni “haramu kabisa.”
Habari ID: 3482238 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/14
IQNA – Papa Leo XIV amemtunuku Hujjatul‑Islam Mohammad Hossein Mokhtari, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Vatican, nishani ya juu zaidi ya kidiplomasia ya Vatican.
Habari ID: 3482235 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/13
IQNA – Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni wa Israel vimegeuza mitaa mizima ya mji wa Gaza kuwa magofu ya simenti na vyuma vilivyopinda.
Habari ID: 3482219 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/09