IQNA

Qari Kutoka Cameroon asoma Surah An-Nasr kwa ajili ya Kampeni ya Fath ya Qur’ani

20:07 - August 07, 2025
Habari ID: 3481049
IQNA – Ahmad Al-Daleel, msomaji na mhifadhi mahiri wa Qur’ani Tukufu kutoka Jamhuri ya Cameroon, ameungana na kampeni ya Fath ya Qur’ani kwa kuwasilisha video ya kisomo chake cha kuvutia cha Surah An-Nasr.

Kampeni hii, iliyoanzishwa na Shirika la Kimataifa la Habari za Qurani (IQNA), inahamasisha Waislamu kushiriki kwa kusoma aya maalum za Qurani Tukufu – ikiwemo Surah Al-Fath (aya 1–4), Surah An-Nasr, na aya ya 139 ya Surah Al-Imran.

Waandalizi wanasema usomaji huu unalenga kuwa nguvu ya kiroho kwa wapiganaji walioko mstari wa mbele, na pia kukuza ujumbe wa Qurani wa subira, msaada wa Mwenyezi Mungu, na ushindi wa haki juu ya batili.

Tuma usomaji wako kwa WhatsApp kupitia nambari: +989127397608

captcha