IQNA

Waislamu Malaysia waunga mkono mitazamo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

14:05 - January 19, 2026
Habari ID: 3481821
IQNA – Baraza la Mashauriano la Mashirika ya Kiislamu Malaysia (MAPIM) limetoa tamko likieleza kuunga mkono msimamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kuhusu kumweka rais wa Marekani kuwa na dhima juu ya vifo na uharibifu uliotokana na machafuko ya hivi karibuni nchini Iran.

Matukio ya karibuni nchini Iran yanaweza kutathminiwa ndani ya muktadha wa muundo unaojulikana wa mwingilio wa kigeni, upangaji wa nyuma ya pazia, na kutumia maandamano kama silaha; mwenendo ambao, kwa mujibu wa tamko hilo, umechangia mateso na madhara makubwa kwa raia katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Kile kilichoonekana katika machafuko ya hivi karibuni nchini Iran ni mgeuko wa maandamano ya kiraia na ya amani kuelekea vitendo vya vurugu, mashambulizi dhidi ya raia, maafisa wa usalama, na miundombinu ya umma; mchakato ambao, ikiwa unaelekezwa au kuungwa mkono na mashirika ya kijasusi ya kigeni, hugeuka kuwa zana ya vita vya kijiopolitiki, linasisitiza tamko hilo.

MAPIM pia ilieleza wasiwasi mkubwa kuhusu matamko na ujumbe uliotolewa na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo, pamoja na taasisi ya kijasusi ya utawala wa Israeli, katika kuunga mkono machafuko hayo na hata kudai kuwa na uwepo wa moja kwa moja katika maeneo ya tukio. MAPIM ilitaja hatua hizo kuwa ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya kitaifa ya nchi na pia kinyume na sheria za kimataifa.

Taasisi hiyo imekosoa undumakuwili na unafiki wa wale wanaodai kuwa watetezi wa demokrasia, na kuongeza kwamba: “Kuitisha au kuhimiza kuvurugika kwa uthabiti wa nchi nyingine, kunakofanywa na wahusika wanaokandamiza maandamano ndani ya mipaka yao wenyewe na kukaa kimya mbele ya ukaliaji wa mabavu, mzingiro, na uhalifu wa kivita, ni ishara ya matumizi ya dhana ya uhuru kama chombo cha maslahi.”

Habari inayohusiana:

Katika hotuba yake siku ya Jumamosi, Ayatullah Khamenei alilisifu taifa la Iran kwa, kama alivyosema, kufanikiwa kuvunja nguvu za fitina wakati wa machafuko ya hivi karibuni. Pia alimtaja Rais wa Marekani, Donald Trump, kuwa ni mhalifu kwa kusababisha madhara dhidi ya taifa la Iran.

Habari zinazohusiana
captcha