IQNA

Kiongozi wa Yemen asema Marekani imefedheheka baada ya kuibua ghasia Iran

14:59 - January 23, 2026
Habari ID: 3481834
IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema Marekani ilichochea machafuko ya hivi karibuni nchini Iran, na kwamba imefedheheka kwani njama za zimepata kipigo kikubwa cha kimkakati.

Abdul Malik al‑Houthi ameisitiza kuwa Marekani “imepata misukosuko mikubwa na kushindwa kwa fedheha” baada ya kuchochea ghasia za kigaidi ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bila kufanikisha malengo yake maovu.

Katika hotuba yake ya Alhamisi, al‑Houthi alisema njama ya Washington dhidi ya Iran imekuwa ya kina na ya muda mrefu, lakini hatimaye “imetibuka kabisa,” na kuacha Marekani ikiwa imepata kile alichokitaja kama kushindwa kwa kiwango cha juu.

Alisema kwamba “kulengwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani kulikuwa kwa kiwango cha juu, lakini kumeanguka kabisa, na magenge ya kihalifu yakaporomoka.”

Amekosoa mbinu za Marekani, akieleza kuwa taifa hilo lina ustadi wa kutengeneza simulizi zinazochochea misukosuko, kisha kulitumia ghasia zinazoibuka kwa maslahi yake ya kisiasa na kiuchumi, mtindo ambao mara nyingi huonekana katika siasa za eneo la Asia ya Magharibi.

Kile kilichoanza mwishoni mwa mwezi uliopita kama maandamano ya amani katika Soko Kuu la Tehran, mwito wa mageuzi ya kiuchumi katikati ya mfumuko wa bei unaopaa na kushuka kwa thamani ya sarafu, kiligeuzwa haraka kuwa vurugu.. Magaidi waliopatiwa mafunzo na CIA na Mossad waliingia miongoni mwa umati ili kuchochea hasira na kugeuza maandamano kuwa vurugu.

Al‑Houthi aliongeza kuwa Marekani na utawala wa Kizayuni wanaendelea kutafuta ushawishi na udhibiti mpana katika eneo zima la Asia ya Magharibi, jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha mvutano katika ukanda huo wenye historia ndefu ya mwingiliano wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni katika Bahari ya Hindi.

Alibainisha kuwa mashambulizi yasiyokoma dhidi ya Yemen yalipangwa na kusukumwa na Marekani, Uingereza na Israel, akisema kuwa mkondo wa vita hivyo haukuwa wa bahati mbaya bali wa mkakati mpana wa kieneo.

Alisema utajiri wa mafuta wa Yemen pamoja na nafasi yake ya kijiografia, mlango muhimu wa Bahari ya Hindi na njia za biashara za kimataifa, vimeifanya nchi hiyo kuwa kitovu cha tamaa za nguvu za kibeberu.

Al‑Houthi alisisitiza: “Lau Wamarekani, Waingereza, Wasaudi na washirika wao wangekuwa wameikalia kikamilifu nchi yetu, wangeitumia nafasi yake ya kimkakati kwa kuweka kambi za kijeshi na kutimiza malengo yao, na wangelinyonya rasilimali zake kubwa ambazo bado hazijaguswa.”

Akaongeza kuwa “kulengwa kwa Yemen kunaendelea kwa sura zote kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono wananchi wa Palestina na kupinga mashambulizi ya Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.”

Kwa mujibu wake, vikosi vya Israel vinaendelea na mashambulizi hatari ndani ya Gaza licha ya tangazo la Marekani kuhusu kuanza kwa awamu ya pili ya usitishaji mapigano.

Alisema kuwa Waisraeli, wakiwa sambamba na Wamarekani, hawatilii maanani makubaliano ya usitishaji mapigano wala makubaliano mengine, hata yale yenye dhamana na masharti yaliyo wazi.

Al‑Houthi alisema kuwa “baraza linalodaiwa la Trump linatafuta utawala wa mabavu, vitisho, ukandamizaji, kujilimbikizia mali, na kunyakua maslahi na rasilimali za taifa la Palestina.”

Habari zinazohusiana:

Alilaani uvamizi mpana wa Israel katika maeneo ya kusini mwa Lebanon pamoja na udhibiti wa Israel katika sehemu za kusini mwa Syria, akisema kuwa hatua hizo zinaendeleza mnyororo wa mvutano katika ukanda wa Asia ya Magharibi.

Alisisitiza kuwa Marekani “inalenga eneo zima ndani ya mradi wa Kizayuni na inatafuta kuhakikisha kuwa wanaoshika nyadhifa za juu wanatumikia maslahi ya Marekani na Israel.”

Kiongozi huyo wa Yemen aliongeza kuwa “hakuna utawala wa Kiarabu unaoweza kuchukua nafasi ya Israel kama wakala mkuu wa Marekani katika eneo, haijalishi unatoa fedha au huduma kiasi gani.”

Katika hotuba hiyo, al‑Houthi alieleza kuwa Marekani imekuwa ikiilenga Venezuela na mataifa mengine ya Amerika ya Kusini kwa miongo kadhaa kupitia ukandamizaji, uporaji wa rasilimali, na kuingilia mambo yao ya ndani.

Alisema Wamarekani wamekuwa wakionyesha vitendo vya mabavu kwa uwazi zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Aidha, alifafanua kuwa Marekani inatafuta kudhibiti Greenland, licha ya tayari kuwa na kambi za kijeshi na upatikanaji wa wazi wa maslahi ya kiuchumi kupitia Denmark pamoja na mamlaka na wakaazi wa kisiwa hicho.

“Amerika haitosheki na uwepo na upatikanaji—inataka umiliki kamili,” al‑Houthi alisema.

3496150

 

 

3496150

captcha