IQNA

Wito wa kufanyika uchunguzi baada ya maneneo ya Chuki dhidi ya Uislamu kuandikwa Missouri

12:00 - May 26, 2026
Habari ID: 3482284
IQNA – Wakazi wa kitongoji kilichopo kusini mwa Kaunti ya St. Louis, jimboni Missouri nchini Marekani, wameamka mwishoni mwa wiki wakikuta mandhari ya kutia hofu, baada ya njia za waenda kwa miguu na baadhi ya barabara kuchafuliwa kwa maandishi ya chuki dhidi ya Waislamu.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) siku ya Jumatatu lililaani vikali vitendo hivyo vya chuki vinavyolenga Waislamu katika eneo la kusini mwa St. Louis County, na kutoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.

Kwa mujibu wa ripoti za ndani, polisi wanaendelea kuchunguza matukio kadhaa yaliyohusisha ujumbe wa chuki dhidi ya Waislamu na wahamiaji katika maeneo yaliyoathirika.

Katika taarifa yake, CAIR yenye makao yake makuu Washington, D.C., ilisema:

“Tunalaani kwa nguvu zote vitendo hivi vya chuki na vitisho dhidi ya Waislamu vinavyowalenga wakazi wa Missouri. Uharibifu unaochochewa na ubaguzi pamoja na matamshi ya chuki huchangia kuibua mazingira ya hofu na mgawanyiko yanayotishia usalama na ustawi wa Waislamu wa Marekani pamoja na jamii nyingine za wachache. Tunazitaka mamlaka za utekelezaji wa sheria kufanya uchunguzi wa kina na kuwawajibisha waliohusika.”

CAIR ilibainisha kuwa ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu haki za kiraia ilirekodi malalamiko 8,683 ya ubaguzi dhidi ya Waislamu katika mwaka 2025, idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa na taasisi hiyo tangu ilipoanza kuchapisha ripoti hizo mwaka 1996.

Aidha, Kituo cha Utafiti wa Chuki Iliyopangwa (Center for the Study of Organized Hate) kilieleza kuwa kumekuwa na ongezeko la takriban asilimia 1,450 la matamshi yenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu kutoka kwa baadhi ya viongozi wa umma katika kipindi cha miezi 15 baada ya Februari 2025. Kituo hicho kilionya kuwa kauli nyingi kama hizo zinaweza kuchochea vitendo vya vurugu.

CAIR pia imewataka viongozi wa jamii za Kiislamu kutumia kijitabu chake kiitwacho “Best Practices for Mosque and Community Safety” yaani “Mbinu Bora za Usalama wa Msikiti na Jamii” ili kusaidia kuimarisha usalama wa misikiti na vituo vya kidini. Shirika hilo limeeleza kuwa mwongozo huo unaweza kutumika katika 

3497604

captcha