Mmiliki wa klabu hiyo, Alex Haditaghi, alilinganisha kufanya biashara na klabu ya Israel na kufanya biashara na Ujerumani ya Nazi.
Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Haditaghi alisema ameiarifu Maccabi Tel Aviv kuhusu uamuzi wake wa kutokuendelea na mazungumzo ya uhamisho wa mabeki Dimitris Keramitsis na Leo Borges.
Katika barua aliyomwandikia rais wa klabu ya Israel na kuichapisha kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii, Haditaghi alisema kuwa soka linapaswa kuwakilisha “matumaini, heshima, umoja na ubinadamu,” na linapaswa kuwa “juu ya siasa, mipaka au migawanyiko.”
Hata hivyo, alisema mateso yanayoendelea kuwafika raia wasio na hatia huko Gaza, Lebanon, Iran na maeneo mengine ya eneo hilo yanaifanya isiwe sahihi kwa klabu yake kufanya biashara na klabu ya Israel kwa wakati huu.
“Kwa kuzingatia mateso yanayoendelea ya raia wasio na hatia huko Gaza, Lebanon, Iran na katika eneo zima, na pia kwa kuzingatia vitendo vya vurugu, mauaji ya halaiki na ukosefu wa ubinadamu vinavyofanywa na dola ya Israel, siamini kuwa itakuwa sahihi kimaadili kwa klabu yetu kuendelea na muamala wowote wa kibiashara na klabu inayoiwakilisha Israel kwa wakati huu,” aliandika.
Haditaghi alisema wajibu wake hauishii tu katika maslahi ya kifedha ya klabu, bali pia unahusu kulinda “maadili, misingi na ubinadamu.”
“Kama ningekuwa hai katika nyakati za Ujerumani ya Nazi, mojawapo ya vipindi vibaya zaidi katika historia ya mwanadamu, nisingefanya biashara na klabu yoyote ya michezo iliyokuwa ikiuwakilisha utawala wa Nazi — utawala uliowajibika kwa mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya mamilioni ya watu wasio na hatia,” aliandika.
“Leo hii nalazimika kutumia kipimo hichohicho cha maadili.”
“Zipo nyakati ambapo maadili yanapaswa kuwa na nguvu zaidi kuliko faida na fedha,” aliongeza.
Ofa zilizotajwa zilihusu wachezaji Keramitsis na Borges, ambao mikataba yao na Pogon inaendelea hadi mwaka 2029 na 2027 mtawalia.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukitekeleza jinai na mashambulizi haramu ya kijeshi huko Lebanon, Gaza na Iran ambapo utawala huo umeua makumi ya maelfu ya watu wasio na hatia.
3497739