IQNA-Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa Linalowahudumia Wakimbizi wa Kipalestina ( UNRWA ) amezitaka nchi za Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi kutenga tone tu la fedha zilizotajwa katika ‘makubaliano makubwa’ kati yao na Rais wa Marekani, Donald Trump, ili kusaidia wakimbizi wa Kipalestina wanaopambana kuendelea kuishi katika ardhi zao ambazo Israel imezikalia kwa mabavu na pia wale wanaoishi katika nchi jirani.
Habari ID: 3480762 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/30
IQNA-Mkuu wa Shirika la UN la Wakimbizi wa Palestina ( UNRWA ) ametahadharisha kwamba hatua ya utawala wa Israel kuweka mzingiro na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia katika Ukanda wa Gaza inapelekea eneo hilo la pwani kukaribia baakubwa la njaa.
Habari ID: 3480426 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/24
Mauaji ya Kimbari Gaza
IQNA - Ili kushughulikia mahitaji ya dharura zaidi ya Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina ( UNRWA ) limewasilisha ombi la dharura la msaada wa dola bilioni 1.21.
Habari ID: 3478731 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/25
Kadhia ya Palestina
IQNA-Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA , limeonya kuhusu vifo vingi vya watoto katika Ukanda wa Gaza huku kukiwa na ukosefu mkubwa wa chakula na upatikanaji wa maji salama na huduma za matibabu katika eneo hilo.
Habari ID: 3478456 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/05
Jinai za Israel
IQNA-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina ( UNRWA ) limeonya kwamba mashambulizi ya utawala haramu wa Israel dhidi ya mji wa mpakani wa Rafah wenye msongamano mkubwa wa watu Gaza yatakuwa "kichocheo cha maafa."
Habari ID: 3478326 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/09
Mtazamo
IQNA- Ikiwa imepita miezi minne ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza, utawala huo umeshindwa kufikia lengo la kuangamiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, na pia haujaweza kuvunja azma na irada ya wakazi wa eneo hilo. Hivyo ili kujaribu kufidia kufeli huko, Wazayuni wakishirikiana na baadhi ya waitifaki wao wa Magharibi, sasa wanalenga kusambaratisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA .
Habari ID: 3478288 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/01
Jinai za Israel
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema katika chapisho la ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X jana Jumapili kwamba kukata ufadhili kwa UNRWA "kutawaumiza tu watu wa Gaza".
Habari ID: 3478278 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/30
Jinai za Israel
IQNA - Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi la Palestina UNRWA amesema kuwa uamuzi wa baadhi ya nchi za Magharibi kusitisha misaada ya kifedha kwa shirika hilo ni sawa na "adhabu ya pamoja" ambayo itapunguza misaada ya kuokoa maisha kwa watu milioni mbili huko Gaza.
Habari ID: 3478265 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/28
Jinai za Israel
IQNA-Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imeashiria mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuwafukuza kwa umati Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kutahadharisha kuwa, pendekezo la viongozi wa utawala huo wa Kizayuni la kutaka kupunguzwa idadi ya wakazi wa Gaza ni jinai ya kivita.
Habari ID: 3478128 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/01
Wakimbizi Wapalestina walio katika nchi mbali mbali duniani wanakabiliwa na matatizo makubwa sana. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina ( UNRWA ) limetoa onyo kuhusu hali mbaya sana ya wakimbizi Wapalestina.
Habari ID: 3023920 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/22