IQNA

Indhari ya UNRWA: Israel itaibua maafa makubwa ya njaa Gaza

18:36 - March 24, 2025
Habari ID: 3480426
IQNA-Mkuu wa Shirika la UN la Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) ametahadharisha kwamba hatua ya utawala wa Israel kuweka mzingiro na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia katika Ukanda wa Gaza inapelekea eneo hilo la pwani kukaribia baakubwa la njaa.

Philippe Lazzarini ameyasema hayo hayo katika chapisho kupitia mitandao ya kijamii, ambapo amesisitiza kwamba mzingiro huo, ambao unazuia chakula, dawa, maji na mafuta kuingia katika eneo hilo, umeendelea kwa muda mrefu.

Israeli imezuia kuingia kwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza tangu Machi 4, kufuatia kumalizika kwa awamu ya kwanza ya mapatano ya kusitisha mapigano na makubaliano na harakati ya Muqawama ya Hamas kuhusu kubadilishana mateka wa Israeli kwa wafungwa wa Kipalestina.

Lazzarini amesema kila siku inayopita bila kuingia kwa msaada ina maana watoto wengi wanakwenda kulala wakiwa na njaa, magonjwa yanaenea na ukosefu wa vitu unazidi kuwa mbaya.

Afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema: “Kila siku bila chakula ina maana Gaza inakaribia baa kubwa ya njaa." Lazzarini amesema kuzuia msaada ni adhabu ya pamoja kwa watu wa Gaza – ambao wengi wao ni watoto, wanawake na wanaume wa kawaida.

Chini ya himaya kamili ya Marekani na washirika wake wa Magharibi, utawala haramu wa Israel ulianza vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, baada ya harakati ya Muqawama ya Hamas kufanya Kimbunga cha Al-Aqsa dhidi ya utawala wa Israel kama jibu kwa kampeni yake ya muda mrefu ya jinai dhidi ya Wapalestina.

Mashambulizi ya kikatili ya utawala huo dhidi ya Gaza hadi sasa yameua Wapalestina wasiopungua 50,021, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi wengine 113,274. Maelfu zaidi pia wametoweka na inaaminika wamekufa chini ya vifusi.

Mnamo Novemba 21 mwaka jana, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ilitoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa vita Yoav Gallant kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika Gaza.

Israeli pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa vita vyake vya kikatili dhidi ya Gaza.

3492479

Habari zinazohusiana
captcha