iqna

IQNA

Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema Waislamu ni waathirika wakuu wa ugaidi duniani.
Habari ID: 3470236    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/04/09

Mfalme Abdullah II wa Jordan ameituhumi Uturuki kuwa inahimiza misimamo mikali eneo la Mashariki ya Kati sambamba na kueneza magaidi bara Ulaya.
Habari ID: 3470219    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/28

Donald Trump, mwanasiasa wa chama cha Republicans amesema baadhi ya waitifaki wa Marekani, ikiwemo Israel, wanaliunga mkono na kulipa misaada kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
Habari ID: 3463979    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/16

Idadi ya raia wa kigeni waliojiunga na makundi ya magaidi wakufurishaji nchini Syria wameongezeka maradufu, amesema mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Uingereza.
Habari ID: 3461648    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/09

Mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu nchini Russia amesema misikiti 7,500 mipya imejengwa nchini humo wakati wa kipindi cha urais wa Vladimir Putin.
Habari ID: 3461608    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/09

Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia ametangaza hali ya hatari ya siku 30 kufuatia shambulizi dhidi ya basi lililokuwa limewabeba maafisa usalama wa nchi hiyo hapo .jana
Habari ID: 3457119    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/25

Ayatullah Ahmad Khatami
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa wiki mjini Tehran amesema kundi la kigaidi la Daesh au ISIS matakfiri kwa ujumla ni mamluki wa Wazayuni ambao wametumwa kwa lengo la kuwagombanisha Waislamu.
Habari ID: 3454898    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/21

Rais Rouhani
Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ufaransa wametangaza utayarifu wa nchi hizo mbili kwa ajili ya kushirikiana katika masuala ya usalama na habari za kipelelezi katika fremu ya mapambano dhidi ya ugaidi.
Habari ID: 3454175    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/18

Kiongozi mmoja anayejihusisha na harakati za kusimamia haki za Waislamu na wahajiri waishio katika viunga vya jiji la Paris, Ufaransa ameonya juu ya kushadidi wimbi kubwa la chuki dhidi ya Waislamu kutokana na mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Habari ID: 3451758    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/15

Watu wasiopungua 160 wameuawa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris Ijumaa usiku katika mashambulizi yanayosadikiwa kuwa makubwa zaidi nchini humo tangu baada ya Vita vya Pili vya Dunia.
Habari ID: 3448027    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/14

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani shambulio la ugaidi lililofanywa na kundi la kitakfiri la ISIS au Daesh nchini Lebanon siku ya Alhamisi ambapo watu 43 waliuawa na wengine zaidi ya 240 wamejeruhiwa.
Habari ID: 3447662    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/13

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (ISESCO) limelaani vikali hujuma ya kigaidi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa katika majlisi ya maombolezo ya siku 10 za Muharram nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3388672    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/18

Mufti Mkuu wa Tunisia amesema kuwa mirengo yenye kufurutu ada na makundi ya kitakfiri kama ISIS au Daesh ni tishio kuu kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3386403    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/17

Waislamu watano wa madhehebu ya Shia wameuawa nchini Saudi Arabia kufuatia hujuma ya kundi la kigaidi la Daesh au ISIS katika majlisi ya maombolezo ya siku 10 za Muharram.
Habari ID: 3386096    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/17

Kinara wa kundi la kigaidi la Daesh au ISIS, Abubakar al-Baghdadi amejeruhiwa katika hujuma ya Jeshi la Anga la Iraq..
Habari ID: 3384677    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/12

Rais wa Iran na Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu wametoa ujumbe tofauti kufuatia kuuawa shahidi Brigedia Jenerali Hussein Hamedani katika vita dhidi ya magaidi na kutoa mkono wa pole kwa wananchi wa Iran.
Habari ID: 3383361    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/09

Magaidi wa kundi la ISIS au Daesh wameshambulia kwa bomu Masjid Nur jana Jumanne katika mtaa wal al-Nahda katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a ambapo watu saba wamepoteza maisha.
Habari ID: 3382986    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/07

Waislamu 25 wa madhehebu ya Shia wameuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a baada ya bomu kulipuka ndani ya msikiti wakati wa Swala ya Idul-Adh’ha mapema leo asubuhi.
Habari ID: 3367085    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/24

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Nickolay Mladenov Mashariki ya Kati amesema kunahitajika muungano wa kimatiafa wa kijeshi ili kuangamiza kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
Habari ID: 3363344    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/16

Maulamaa Waislamu zaidi ya 1,000 nchini India wametoa Fatwa ya pamoja kulaani na kupinga kundi la kigaidi la ISIS au Daesh na kusema harakati za kundi hilo ni dhidi ya mafundisho ya Kiislamu.
Habari ID: 3361079    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/10