IQNA

Raia 31,000 wa kigeni wajiunga na makundi ya kigaidi Syria

12:58 - December 09, 2015
Habari ID: 3461648
Idadi ya raia wa kigeni waliojiunga na makundi ya magaidi wakufurishaji nchini Syria wameongezeka maradufu, amesema mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Uingereza.

Richard Barrett mkuu wa zamani wa kitengo cha kupambana na ugaidi wa kimataifa katika Shirika la Kijasusi la Uingereza la M16 amesema raia 31,000 wa kigeni wameingia Syria na kujiunga na makundi ya kigaidi katika kipindi cha miezi 18 iliyopita.
Amebainisha kuwa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh ndilo linalowavutia wapiganaji wa kigeni. Barrett ambaye hivi sasa ni afisa mwandamizi wa Shirika la Ushauri wa Kiintelijensia la Soufan mjini New York amesema watu wengi zaidi wanajiunga na ISIS pamoja na kuwepo jitihada za kuangamiza kundi hilo la kigaidi.
Magaidi kutoka nchi 86 kuanzia Norway hadi Uzbekistan hadi Mashariki ya kati na baadhi ya nchi za Kiafrika. Aghalabu ya magaidi waliojiunga na makundi ya wakufurishaji Syria na Iraq ni kutoka Tunisia, Saudi Arabia, jamhuri za zamani za Shirikisho la Sovieti huku magaidi takribani 5,000 wakiwa wametoka nchi za Ulaya.

3461289

captcha