iqna

IQNA

Maulamaa Waislamu Ghana
Maulamaa wa Kiislamu nchini Ghana wametangaza msimamo wa kupinga vikali kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na kutoa wito kwa vijana nchini humo kuisoma na kufahamu ipasavyo tafsiri ya Qur'ani kwa njia sahihi ili wasitumbukie katika mtego muovu wa ISIS.
Habari ID: 3360612    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/08

Kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) limetekeleza miripuko ya mabomu kwenye msikiti wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia katika mji mkuu wa Yemen Sana'a na kupelekea waumini wasiopungua 32 kupoteza maisha.
Habari ID: 3357626    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/03

Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limeweka sheria kali kwa wakaazi wa mji wa Mosul, Iraq ambao wanataka kuelekea katika safari ya kila mwaka ya ibada ya Hija.
Habari ID: 3354583    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/31

Kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS(Daesh) nchini Iraq, limebomoa msikiti mmoja kusini mwa mkoa wa Nainawa, sanjari na kuondoa nakshi za kihistoria katika makanisa mawili katikati ya mji wa Mosul.
Habari ID: 3353853    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/30

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ameelezea masikitiko yake kuhusu kimya cha Umoja wa Mataifa na taasisi zingine za kimataifa kuhusu mauaji yanayoendelea dhidi ya watu wasio na hatia nchini Yemen.
Habari ID: 3353340    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/29

Kundi la magaidi na wakufurishaji wa ISIS (Daesh) kwa mara nyingine wametishia kuibomoa al-Ka'aba katika mji mtakatifu wa Makka.
Habari ID: 3353091    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/27

Wanazuoni wa Kiislamu leo wamemaliza kikao chao Misri ambapo wamejadili ‘fatwa za misimamo mikali’ ambazo zimekuwa zikitolewa na makundi ya kigaidi hasa kundi la kitakfiri la Daesh (ISIS).
Habari ID: 3345846    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/18

Mshtakiwa muhimu zaidi wa shambulio la kigaidi ndani ya msikiti mmoja nchini Kuwait amekiri kuwa ni mwanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.
Habari ID: 3339565    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/06

Kundi la kigaidi na Kitakfiri la Daesh (ISIS) limetangaza kuwapiga marufuku Waislamu kusali Sala ya Idul Fitr baada ya kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3327619    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/13

Baraza Kuu la Maulamaa wa Kiislamu nchini Sudan wametangaza kuwa ni haramu kujiunga na makundi yenye misimamo mikali ikiwemo kundila kigaidi la Daesh au ISIS.
Habari ID: 3325723    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/07

Ayatullah Muhsin Araki
Waislamu duniani wametakiwa wasisahau kadhia ya kupigania ukombozi wa Palestina katika kipindi hiki ambapo wengi wanajishughulisha na tatizo sugu la ugaidi na jinai zinazotekelezwa na kundi la kigaidi na kitakifiri la Daesh au ISIS.
Habari ID: 3322212    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/01

Serikali ya Tunisia imeamua kufunga misikiti 80 inayoendeshwa nje ya udhibiti wake, siku moja baada ya kutokea shambulio la kigaidi na kupelekea makumi ya watu kuuawa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Habari ID: 3320222    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/28

Watu wasiopungua 25wameuawa kufuatia hujuma ya kigaidi iliyolenga msikiti wa Imam Sadiq AS katika mji wa Kuwait.
Habari ID: 3319688    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/26

Magaidi wa kundi la Kitakfiri la Daesh au ISIS wamebomoa makaburi mawili ya kale ya Mawalii wa Allah SWT katika mji wa kihistoria wa Palmyra mkoani Homs nchini Syria.
Habari ID: 3318384    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/24

Hata baada ya kupita miezi kadhaa ya kusonga mbele kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika medani za vita kwenye nchi za Kiislamu, Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa serikali ya Washington bado haina stratijia kamili ya kukabiliana na kundi hilo.
Habari ID: 3313196    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/11

Mwenyekiti wa Maulamaa wa Ahlu Sunna nchini Iraq amesema kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) ni wajibu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Habari ID: 3310587    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/02

Sayyid Hassan Nasrullah
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, harakati za kundi la kitakfiri na kigaidi la Daesh (ISIS) zinatekeleza kikamilifu malengo ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 2862976    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/17