iqna

IQNA

Mahojiano
IQNA - Kamanda katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amesema Jamhuri ya Kiislamu haitajihusisha na vita vya moja kwa moja na utawala haramu wa Israel na kwamba jibu la shambulio la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria halitakuwa kwa  makombora na ndege zisizo na rubani pekee.
Habari ID: 3478653    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/08

Vita dhidi ya ugaidi
IQNA-Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa, limevurumisha makombora ya balestiki kulenga ngome za magaidi wa Syria, waliohusika katika mashambulizi ya hivi karibuni nchini Iran, pamoja na kituo cha ujasusi cha Israel katika eneo la Kurdistan ya Iraq.
Habari ID: 3478201    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/16

Vita dhidi ya magaidi
TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Rais wa Syria imetoa taarifa ikizungumzia kushindwa ugaidi mbele ya irada na uwezo wa nchi hiyo na kusisitiza kwamba damu ya Mashahidi wa chuo cha kijeshi cha Homs inaongeza azma ya Damascus ya kufikia ushindi kamili.
Habari ID: 3477693    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/06

Uchambuzi
TERHAN (IQNA)- Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu walikubaliana katika mkutano wao waliofanya Jumapili tarehe 7 Mei mjini Cairo kurejeshwa Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League), baada ya kusimamishwa uwanachama wake kwa muda wa takriban miaka 12.
Habari ID: 3476982    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/09

Diplomasia
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea ziara yake ya siku mbili nchini Syria kama hatua ya mabadiliko katika kukuza uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama baina ya nchi mbili na kuongeza kuwa lengo kuu la safari hiyo lilikuwa ni kuenzi muqawama au mapambano ya serikali na taifa la Syria.
Habari ID: 3476962    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/05

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ametaja kufeli Marekani katika kuziunganisha nchi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni ushindi au nusra kutoka kwa Mwenyezi Mungu na akaongeza kuwa: "Kumfuata Wali ul Amr wa Waislamu na Hujja za Kisharia ni mfano wa usaidizi wa Mwenyezi Mungu."
Habari ID: 3476960    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/05

Diplomasia
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, serikali ya Syria pamoja na wananchi wa nchi hiyo wamepitia masaibu na matatizo mengi na hii leo taifa hilo limeweza kupata ushindi.
Habari ID: 3476950    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/03

Hali nchini Syria
TEHRAN (IQNA)- Ujumbe wa maspika na wabunge wa mabunge ya nchi za Kiarabu uliwasili Damascus, mji mkuu wa Syria siku ya Jumapili kuonyesha mshikamano na nchi hiyo kufuatia matetemeko makubwa ya ardhi yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu nchini Syria na Uturuki.
Habari ID: 3476631    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/27

Zilzala Uturuki na Syria
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amefanya ziara rasmi nchini Uturuki kufuatia matetemeko makubwa ya ardhi yaliyoikumba nchi hiyo zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Habari ID: 3476606    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/22

Ugaidi wa Marekani
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali jinai ya hivi karibuni ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh katika viunga vya mji wa Homs nchini Syria na kusema: "Utawala wa Marekani unafuatilia sera za undumakuwili katika masuala ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi."
Habari ID: 3476586    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/19

Zilzala Syria na Uturuki
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein AS imetuma timu ya madaktari kaskazini mwa Syria kwa ajili ya kutoa misaada kwa wale walioathiriwa na mItetemeko mkubwa ardhi.
Habari ID: 3476580    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/18

Jinai ya magaidi
TEHRAN (IQNA)- Raia wasiopungua 53 wameuawa katika shambulio linaloaminika kufanywa na magaidi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika mkoa wa Homs, magharibi mwa Syria.
Habari ID: 3476579    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/18

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) – Takriban misikiti miwili mjini London imepokea barua za chuki dhidi ya Uislamu kufuatia mitetemeko mikubwa ya ardhi nchini Uturuki na Syria ambayo imesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu.
Habari ID: 3476576    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/17

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amekosoa mienendo ya nchi za Magharibi kuhusiana na tetemeko la ardhi nchini Syria.
Habari ID: 3476573    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/17

Zilzala Uturuki na Syria
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) ametoa wito kwa Waislamu walionuia kutekeleza safari ya ibada ya Hija ndogo ya Umrah kusitisha safari hiyo kwa sasa na badala yake kutumia fedha hizo kuwasaidia wahanga wa mitetemeko (zilzala) ya ardhi Uturuki na Syria.
Habari ID: 3476559    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/14

Zilzala Syria na Uturuki
TEHRAN (IQNA)-Matumaini ya kupata manusura zaidi chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa mitetemeko miwili mikubwa ya ardhi Jumatatu iliyopita katika nchi za Syria na Uturuki yanazidi kupungua siku 5 baada ya maafa hayo ambapo idadi ya walipoteza maisha hadi sasa ikifika 25,000 huku Umoja wa Mataifa ukitabiri kuwa yamkini idadi hiyo ikaongezeka maradufu.
Habari ID: 3476547    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/11

Misaada kwa Syria
TEHRAN (IQNA)- Shehena ya tano ya misaada ya kibinadamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa watu waliokumbwa na mitetemeko ya ardhi nchini Syria iliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Damascus mapema leo Alhamisi.
Habari ID: 3476537    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/09

Rais Assad wa Syria
TEHRAN (IQNA)- Rais Bashar al-Assad wa Syria amefichua kuwa Marekani inatoa mashinikizo kwa nchi zinazotaka kuwasaidia waathirika wa mitetemeko ya ardhi nchini Syria. Assad ameyasema hayo katika mkutano na ujumbe wa mawaziri kadhaa wa Lebanon.
Habari ID: 3476535    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/09

Zilzala Syria na Uturuki
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza hali ya dharura katika mikoa 10 iliyotikiswa na mitetemeko miwili ya ardhi ambayo imepelekea zaidi ya watu 5,100 kupoteza maisha nchini Uturuki na Syria.
Habari ID: 3476524    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/07

Taazia
TEHRAN(IQNA)- Watu wasiopungua 2,500 wamepoteza maisha kutokana na mitetemeko miwili mkubwa ya ardhi iliyoyakumba maeneo ya kusini mashariki mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria huku idadi ya wahanga wa janga hilo ikiongezeka kila sekunde kutokana na mamia ya watu kufunikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Habari ID: 3476519    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/06