Araghchi amesisitiza msimamo wa kimsingi wa Iran katika kuunga mkono serikali ya Syria na kubainisha kwamba Syria imekabiliwa na mambo magumu zaidi kabla na ina uwezo wa kupata ushindi.
Waziri Araqchi amezitathmini harakati za hivi karibuni za makundi ya kigaidi kuwa ni sehemu ya njama za maadui wa eneo hili na ni dalili ya kwenda sambamba malengo maovu ya magaidi na malengo ya Marekani na Israel ya kuendelea kuzusha vita, kuyumbisha usalama wa eneo hili, na kufidia kushindwa kwa Wazayuni na muqawama.
Kwa upande wake Rais wa Syria Bashar al-Assad amesisitiza kuwa Syria, kama taifa, jeshi na watu, inaendelea kupambana na magaidi.
Rais wa Syria amepongeza misimamo ya uwajibikaji ya Iran katika kuunga mkono usalama na uthabiti wa eneo hususan Syria na kusisitiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano baina ya nchi zote za eneo hili ili kutokomeza ugaidi.
Baada ya kuondoka Syria, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran tayari amewasili Ankara nchini Uturuki ikiwa muendelezo wa safari yake ya kieneo yenye lengo la kujadilii matukio ya hivi karibuni katika eneo hususan nchini Syria.
4251716