Kituo cha Ajib kimeripoti kuwa, mwanamke huyo alishambuliwa akiwa pamoja na watoto wake wanne kwenye duka moja kubwa katika mji wa Troyes.
Watu hao waliomshambulia awali walivunjia heshima na kutusi dini tukufu ya Uislamu na kisha wakampiga mwanamke huyo wakitaka kumvua vazi lake la hijabu.
Maafisa wa dula hilo kubwa walioshuhudia tukio hilo walimsaidia mwanamke huyo Muislamu na kumtoa mikononi mwa wahalifu.
Mwanamke huyo amewasilisha malalamiko polisi ambayo tayari imeanza uchunguzi.
Mwanamke huyo amepewa likizo ya mapumziko kutokana na majeruhi yaliyosababishwa na shambulizi hilo. 1310070